Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Duniani watoa wito wa kusaidiwa taifa la Palestina

Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu Duniani umezitaka nchi za Kiislamu kuchukua hatua ya kulisaidia taifa la Palestina dhidi ya jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Ali al-Qaradaghi, Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Duniani (IUMS) jana Alkhamisi aliashiria jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kuutaka Umma wa Kiislamu kusimama kidete kukabiliana na utawala huo ili kuwasaidia ndugu zao katika eneo hilo la Palestina.

Prof. Ali Muhyiddin Ali Al-Qaradaghi amekosoa kimya cha mashirika ya kiraia na ya kutetea haki za binadamu kuhusiana na jinai za utawala wa Kizayuni na kuongeza kuwa, kukaa kimya ni kushirikiana na kushiriki katika uhalifu unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel.

Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu pia amezitaka nchi zenye nguvu duniani kuuwekea mashinikizo utawala wa Kizayuni ili ukomeshe mauaji ya kimbari.

Karibu Wapalestina elfu khamsini wameuawa shahidi katika mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Isarel huko Palestina.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *