Shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeitaja Vetoi kuwa ni maazimio ya Baraza la Usalama la Marekani kinyume na ombi la nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni wa kuwalinda raia.
Iwapo Marekani itaishinikiza Israel kuwalinda raia katika vita vya Gaza, basi inapaswa pia kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa kukabiliana na mauaji ya raia. Huu ni msimamo wa hivi punde wa shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu katika kujibu kura ya turufu ya maazimio ya Baraza la Usalama kuhusu vita vya Gaza.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema Marekani inapaswa kutumia kiti chake katika Baraza la Usalama kuunga mkono kupitishwa na utekelezaji wa maazimio ya Baraza la Usalama la kuitaka Israel na makundi yenye silaha ya Palestina kukomesha ukiukaji wao wa sheria za vita ambazo zimegharimu maelfu ya maisha ya raia.
Amerika imekuwa muungaji mkono mkuu wa utawala wa Tel Aviv tangu kuanza kwa mashambulizi ya kijeshi ya Israel huko Gaza na imesaidia kuchochea vita kwa kutuma silaha na uungaji mkono wa kisiasa.
Tangu mwanzoni mwa karne ya 21, Washington imepiga kura ya turufu kwa jumla ya maazimio 14 ya Baraza la Usalama ya kuunga mkono utawala wa Kizayuni, ambapo maazimio mawili ya mwisho yanahusiana na usitishaji vita wa hivi karibuni wa Ghaza.
Human Rights Watch pia ilikosoa kile ilichokiita “kiwango maradufu” katika ufuasi wa Washington kwa sheria za vita.
Undumilakuwili wa Wamagharibi katika matukio mengi, ikiwa ni pamoja na kulinganisha utendaji wao nchini Ukraine na Palestina, umevutia hisia, akiwemo Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Alhamisi, akizungumzia suala hilo hilo, na kusisitiza, “Kiwango cha uharibifu wa vita vya Ukraine dhidi ya uharibifu Ukanda wa Gaza si kitu, lakini watu wa Magharibi hawazungumzii kuhusu Gaza.”