Bunge la Knesset (Bunge) la utawala wa Kizayuni kwa mara nyingine tena lilipinga kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina.
Wabunge wa Bunge la Kizayuni walipiga kura kupinga mpango wa kuanzishwa taifa la Palestina kwa wingi wa kura.
Bunge la Kizayuni liliidhinisha mpango huo dhidi ya Palestina kwa wajumbe 68 wa bunge hilo akiwemo Benny Gantz, kiongozi wa chama cha Ittihad dhidi ya kura 9 za kuupinga.
Vyama vya muungano tawala viliunga mkono mpango huu, lakini wanachama wa chama cha “Yesh Atid” kinachoongozwa na “Yair Lapid” waliondoka kwenye kikao cha kupiga kura sambamba na kukataa kwao kuunga mkono mpango huu.
Kwa mujibu wa ripoti hii, katika mpango huu uundwaji wa taifa la Palestina ulipingwa vikali na hatua hiyo ilizingatiwa kuwa ni tishio lililopo kwa utawala wa Kizayuni.
Hapo awali, Bunge la Knesset lilipitisha azimio mwezi Februari ambalo lilikataa kuanzishwa kwa taifa la Palestina kwa upande mmoja. Hata hivyo, Juni 15, bunge la Slovenia lililitambua taifa huru la Palestina kwa wingi wa kura na kujiunga na nchi za Uhispania, Norway na Ireland ambazo hapo awali zilitambua wazo la kuunda taifa la Palestina.
Kabla ya hapo, Dmitry Polyansky, naibu mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa, kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina ni sharti la lazima kwa ajili ya kupatikana amani katika Mashariki ya Kati.
Amesema: Moscow inazitaka nchi zote za dunia kuunga mkono ombi la Palestina la kutaka uanachama wa kudumu katika Umoja wa Mataifa.