Urusi Yaimarisha Ulinzi Katika Daraja La Crimea

URUSI imeimarisha usalama katika daraja lake la pekee linaloiunganisha na eneo la Crimea, baada ya mlipuko mkubwa kuharibu baadhi ya sehemu za daraja hilo Jumamosi.

Rais Vladimir Putin ameagiza Idara ya Usalama wa Mipakani (FSB) kusimamia ulinzi na urekebishaji wa daraja hilo.

Daraja hilo huonekana kuwa ishara ya “ushindi” wa Urusi dhidi Ukraine katika kuliteka eneo la Crimea kuanzia 2014.

Maafisa wa usalama walisema kuwa mlipuko huo uliwaua watu watatu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *