Ushawishi wa Kizayuni katika sinema za Amerika

Faraan: Wazayuni wana ushawishi mkubwa mno katika sinema za “Marekani” kiasi kwamba Mustafa Akkad ambaye ni mkurugenzi wa filamu inayofahamika kama Al-Risalah au Muhammad Rasoolullah (R) na mmoja kati ya wasanii wachache wa filamu za Kiislamu ambaye pia amekua na uzoefu wa mazingira ya Hollywood na Marekani kwa miaka mingi na amefanikiwa kutengeneza filamu kadhaa akiwa huko, amefichua siri hii akisema kwamba:

Katika Hollywood, kila kitu kinadhibitiwa, hata mada ya sinema. Kuna wazalishaji na wafadhili wa Kizayuni wenye uwezo wa mambo wote ambao hawaruhusu wakurugenzi wote kwa ujumla hata wale wanaojitegemea kuwasilisha fikra zao katika mada ya sinema.

Na ili kuweza kueleza kwa bayana nukta hii iliyoashiriwa hapo juu, Ni muhimu kutazama kwa mukhtasari utawala mkubwa walionao Wazayuni katika nguzo za serikali ya Marekan na utamaduni wake Hollywood ikihesabika miongoni mwa tamaduni hizo. Kuanzia mwaka 1898, Muungano wa Wazayuni wa Marekani uliundwa huko mjini New York mpaka zama ambazo Franklin Roosevelt (1945-1939) alipokuwa Raisi wa Marekani na akaunga mkono kuundwa kwa Israeli huko Palestina mnamo mwezi wa Juni mwaka wa 1939. Na Mwakilishi wa Serikali ya Marekani Pamoja na hatua za Rais ajaye wa Marekani Bw. Harry S. Truman aliyeweka shinikizo kwa serikali ya Uingereza kuwafukuza Wayahudi laki moja hadi Palestina mnamo mwaka wa 1946. Nguvu za Wazayuni wa Kiyahudi nchini Marekani ziliongezeka kiasi kwamba kufikia mwaka 1948, dakika kumi na moja baada ya tangazo la Umoja wa Mataifa la kuanzisha taifa la Israeli huko Palestina, serikali ya Marekani iliitambua rasmi nchi ya Israeli.

Lobi rasmi yenye uwezo wa hali ya juu ya Wazayuni nchini Marekani inayofahamika kam ‘American-Israel Public Affairs Foundation’, ambayo kwa kifupi huitwa AIPAC, hivi leo ina ushawishi mkubwa sana katika Nyanja za siasa na Hollywood kiasi kwamba wengine wameiita (Lobi hiyo) ‘Washington King’ yaani Mfalme wa Washington, na mwandishi mwenye utata Paul Findley, aliyekasirishwa na Wazayuni, anaandika katika kitabu chake maarufu, “They Dare to Speak Out.” Anaeleza kua;

Wanachama wote wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, bila ya ubaguzi, wanafwata na kutii maagizo ya Lobi hiyo; Kwa sababu wengi wao wanaona ya kwamba AIPAC kama mwakilishi wa mfumo wa “Capiston Hill” ijulikanayo kwa jina la (Palace of Congress) yaani Ikulu ya Makngamano, ina nguvu kubwa katika Nyanja za kisiasa ambazo zinawafanya kuwa katika nafasi za mbele katika kushinda au kushindwa kwenye uchaguzi.

Chanzo: Mohammad Hossein Farjonejad, hadithi za Kizayuni za sinema
[1] Jarida la Surah, Kituo cha Sanaa cha Shirika la Propaganda la Kiislamu nambari 3.
[2] Mohsen Asami, “Zionism Lobby in the United States of America”, Qom, Wachapishaji wa Faqih, ‘Faqih Publishers’, mwaka 2005, juz.1 uk. 108 na kuendelea, Sura ya Mwanzo na Kuibuka kwa Lobi ya Wazayuni huko Amerika.
[3]. kamati ya masuala ya umma ya Amerika Israeli, AIPAC
[4] Haroon Yahya (Adnan Ektar), “The Untold and Hidden History of America”, iliyotafsiriwa na kuhaririwa na Nasir Sahib Khalq, Tehran, Hilal Publishing, 2006, juz. 2, uk.104.
[5] Paul Findley, ‘They Dare to Speak Out’ yaani “Wanathubutu kuzungumza Pasi na kujali Mipaka’, iliyotafsiriwa na Haidar Soheili Esfahani, Tehran, Quds Publishing, uk.33

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *