Kamati inayoshughulikia masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye magereza ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imetangaza kuwa utawala huo ghasibu unaendelea kuzuia viwiliwili vya Wapalestina kumi waliouawa shahidi.
Kwa mujibu wa chaneli ya habari ya Quds Al-Akhbariya, Kamati ya Wafungwa wa Palestina imetangaza katika taarifa yake siku ya Alkhamisi kwamba Wapalestina hao waliuawa shahidi wakati wa kutiwa nguvuni au walipokuwa vifungoni katika jela za utawala wa Kizayuni na hadi sasa Wazayuni wanakataa kukabidhi miili yao kwa familia zao.
Wengi kati ya Wapalestina hao waliuawa shahidi kutokana na sera za utawala wa Kizayuni za kudharau na kupuuza makusudi kuwapatia huduma za matibabu wafungwa hao, suala ambalo limekuwa likiendelezwa kwa uratibu maalumu na utawala wa Kizayuni katika miongo ya hivi karibuni.