Utawala wa Kizayuni waondolewa kabisa katika ngazi ya usimamizi na Umoja wa Afrika

Mnamo Februari 2023, wakati wa mkutano wa awali wa Umoja wa Afrika, wajumbe wa Israeli walifukuzwa kutoka kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Afrika.

Afrika Kusini na Algeria, ndio nchi mbili zilizokuwa nyuma katika kuwatenga wawakilishi wa Kizayuni, nakupinga kuwepo kwa utawala wa Kizayuni kuwa mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Afrika.

Kulingana na Le Monde, mwaka mmoja baada ya tukio hili la kidiplomasia, vita katika Ukanda wa Gaza vilimaliza mjadala huu. Afisa mkuu wa Umoja wa Afrika anasema: “Faili kuhusu kibali cha Israel limefungwa.”

“Israel haijaalikwa kwenye mkutano huo,” Abba Kalundo, msemaji wa Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, alisema Jumamosi, Februari 17.

Baada ya muongo mmoja wa juhudi za kidiplomasia na miaka miwili baada ya kuidhinishwa, Tel Aviv ilitengwa kabisa na umoja huo.

Kwa upande mwingine, Umoja wa Afrika ulitandaza zulia jekundu kwa Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mohamed Ashtiyah, ambaye alifurahia pongezi za muda mrefu kutoka kwenye jukwaa la Baraza Kuu la Umoja wa Afrika, ambalo zaidi lilikuwa na nia ya kutetea Palestina.

“Wapalestina wanailinda nchi yao, kama vile nyinyi katika Afrika mmelinda ardhi zenu dhidi ya ukoloni,” Eshtie aliwaambia viongozi wa Afrika katika mkutano huu.

Viongozi wa Kiafrika wamelaani uvamizi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Palestina na kuuona kuwa ni ukiukaji wa wazi kabisa wa sheria za kimataifa za kibinadamu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naldi Pandour alielezea wasiwasi wake “kuhusu kuwepo kwa wawakilishi wa Israel katika ofisi za Umoja wa Afrika katika siku za hivi karibuni.”

Siku ya Jumatano, balozi wa Israel nchini Ethiopia alionekana ndani ya jengo la Umoja wa Afrika. Kulingana na vyanzo kadhaa vya kidiplomasia, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel kwa Afrika, Sharon Barley – mtu ambaye alifukuzwa kutoka Umoja wa Afrika mwaka 2023 – anafanya mikutano ya siri katika mji mkuu wa Ethiopia.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *