Utawala wa Saudi Arabia umemhukumu kifo Profesa maarufu wa Chuo Kikuu kwa kutumia mitandao ya kijamii ya Twitter na WhatsApp kuliunga mkono kundi la Ikhwanul Muslimin na kusambaza habari zinazodaiwa kuwa za uhasama dhidi ya ufalme huo wa Aal Saud unaowakandamiza wapinzani na wanaharakati wa mageuzi nchini humo.
Uamuzi huo dhidi ya Awad al-Qarni, Profesa wa sheria anayeunga mkono mageuzi nchini Saudi Arabia, ulitangazwa katika ripoti iliyochapishwa na gazeti la Guardian jana Jumapili. Nasser, mwana wa kiume wa Profesa Awad Qarni ambaye mwaka jana alitoroka Saudi Arabia na sasa anaishi Uingereza amesema hayo katika gazeti moja la Uingereza kuhusu hukumu aliyokatiwa baba yake na utawala wa Saudia.
Profesa Awad Qarni ambaye alitiwa nguvuni Septemba mwaka 2017 alitajwa na vyombo vya habari vinavyosimamiwa na Saudi Arabia kuwa” mhubiri hatari hata hivyo wapinzani wamesema kuwa Profesa huyo wa Chuo Kikuu mwenye umri wa miaka 65 alikuwa msomi muhimu na aliye na wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii. Awad Qarni hadi sasa alikuwa na wafuasi milioni mbili katika mtandao wa Twitter.
Mashtaka dhidi ya Qarni, ambayo yameishia kwenye hukumu ya kifo, ni pamoja na “kukiri profesa huyo wa sheria kwamba alitumia akaunti ya mtandao wa kijamii chini ya jina lake mwenyewe (@awadalqarni) “katika kila fursa ili kutoa maoni yake.”
Wakati huo huo, hati za mahakama ya Saudi Arabia zimedai kuwa Profesa Qarni akikiri kushiriki katika chat ya WhatsApp na alikuwa akituhumiwa kushiriki katika video ambako alionekana kuisifu harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misrin nk.
Hukumu hiyo dhidi ya profesa huyo wa Saudia imetolewa huku Jumuiya za kutetea haki za binadamu na wanaharakati nchini Saudia wakitahadharisha kuwa utawala wa Riyadh mamlaka mjini Riyadh umekuwa ukiwakandamiza wakubwa wapinzani na wakosoaji wa utawala huo wa kifalme hasa ikizingatiwa kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii na mawasiliano mengine yamepigwa marufuku nchini Saudi Arabia tokea Mohammed bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo ashike hatamu za uongozi mnamo 2017.