Baraza la Manispaa la Bogotá, mji mkuu wa Jamhuri ya Colombia, limebadilisha jina la moja ya mitaa muhimu ya jiji hilo kuuita “Mtaa wa Nchi ya Palestina”.
Pamoja na kwamba Marekani na Uingereza zikiwa ndio waungaji mkono wa jadi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel zinajaribu kuficha jinai za utawala huo bandia kutokana na umiliki wao mkubwa wa vyombo vya habari na propaganda, lakini idadi ya wapenzi na waungaji mkono wa wananchi madhulumu wa Palestina inaongezeka kila uchao katika kila pembe ya dunia.
Kulingana na tovuti ya Palestine News, Baraza la Manispaa la Bogota, mji mkuu wa Jamhuri ya Colombia, limepitisha kwa wingi mkubwa wa kura pendekezo la kuupa moja ya mitaa muhimu ya mji huo jina la “Mtaa wa Nchi ya Palestina”.
Mpango huo uliwasilishwa mwaka jana kwa ajili ya majadiliano ya pamoja na mapitio ya jumla; na kutokana na kushindwa kwa lobi ya Wazayuni ukapitishwa kwa kura nyingi, ambapo hatimaye jana Alhamisi, uliidhinishwa rasmi katika kikao cha baraza la Manispaa ya Bogota kwa kuungwa mkono na wawakilishi wa vyama vingi.
Mwaka jana, Colombia ilipiga kura katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ya kuunga mkono azimio la kuitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) itoe “maoni ya ushauri” kuhusu suala la Israel kuyakalia kwa mabavu maeneo ya Palestina.