Uvamizi wa mamia ya walowezi wa Kizayuni kwenye Msikiti wa Al-Aqsa kwa uungaji mkono mkubwa wa polisi wa utawala huo ghasibu

Walowezi hao wa Kizayuni wameushambulia Msikiti wa Al-Aqsa kutoka Bab al-Maghrabeh Jumapili hii asubuhi kwa uungaji mkono mkubwa wa polisi ya utawala huo.

Ili kuhakikisha usalama wa walowezi wanaovamia, polisi ya Kizayuni imeweka vikosi vyake na vitengo maalum katika eneo la Msikiti wa Al-Aqsa na milango yake ya kuingilia tangu asubuhi.

Idara ya Wakfu wa Kiislamu mjini Jerusalem ilitangaza kuwa, makumi ya walowezi wa Kizayuni walishambulia Msikiti wa Al-Aqswa na kuanza vitendo vya uchochezi katika eneo la msikiti huo na kufanya sherehe za Talmudi katika eneo la Bab al-Rahma mashariki mwa msikiti huo.

Polisi ya Kizayuni inaendelea kuweka vikwazo zaidi vya kuingia waumini katika Msikiti wa Al-Aqsa na kuwanyang’anya vitambulisho baadhi ya waumini.

Wananchi wa Quds wanadai harakati za wananchi kuelekea msikiti huu na kutulia ndani yake, kwa kuzingatia hatari inayoletwa na mipango yao ya kubadilisha utambulisho wa Msikiti wa Al-Aqswa kutokana na kuvamiwa na wavamizi na Wazayuni.

Msikiti wa Al-Aqsa unashuhudia mfululizo wa hujuma na mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni kila siku isipokuwa siku za Ijumaa na Jumamosi kwa ajili ya kuikalia kwa mabavu kamili na mgawanyiko wake wa kimada na kimaeneo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *