Uvundo wa ubaguzi wa rangi waendelea kufichuliwa katika utawala wa kifalme wa Uingereza

Mashambulizi ya watu wa mrengo wa kulia na vyombo vya habari dhidi ya Mwanamfalme Harry, mtoto wa Mfalme wa Uingereza na mkewe Meghan, yameripotiwa kuongezeka baada ya kutangazwa habari za filamu mpya ya Netflix kuhusu maisha ya wanandoa hao.

Katika filamu mpya ya matukio ya kweli (documentary) ya Netflix, mtoto wa Mfalme wa Uingereza na mkewe mwenye ngozi isiyo ya wazungu, wanamkosoa aliyekuwa Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, na kuzungumzia “ubaguzi wa rangi” unatawala mfumo wa kifalme wa nchi hiyo; jambo ambalo limeibua hasira za wanasiasa na vyombo vya habari vinavyounga mkono utawala wa kifalme wa Uingereza.

Kwa kuzingatia kwamba sehemu moja ya filamu hiyo itarushwa hewani wiki ijayo, gazeti la Daily Mail limeandika makala likiitaja “wiki ijayo kuwa ni sumu.” Kulingana na gazeti hilo, kasri la Mfalme wa Uingereza lina wasiwasi kwamba filamu hiyo ya Netflix ambayo limedai imejaa “matusi mabaya,” itaikasirisha familia ya kifalme.

Baadhi ya watu wanaounga mkono ufalme nchini Uingereza wanasema kwamba madhumuni ya matamshi ya Harry na Meghan katika filamu hiyo ni kuangusha utawala wa kifalme katika nchi hiyo.

Wanasiasa kadhaa wa Uingereza, akiwemo mbunge wa Conservative, Bob Seely, wanafanya jitihada za kuwapokonya Harry na Meghan vyeo vyao vyote vya kifalme.

Gazeti la Daily Express pia limeandika kwamba Mfalme Charles na washiriki wengine wa familia ya kifalme ya Uingereza wamekasirishwa sana na vita vipya vya Harry dhidi ya familia hiyo. Kwa mujibu wa gazeti hilo, Guy Opperman, mjumbe katika serikali ya Uingereza, ametoa wito kwa Waingereza wote kususia Netflix.

Hapo awali, Meghan, mke mweusi wa mjukuu wa aliyekuwa Malkia wa Uingereza, aliwahi kuripoti kwamba alikuwa mlengwa wa mienendo ya ubaguzi wa rangi katika utawala wa kifalme wa Uingereza na kufikia hatua ya kutaka kujiua.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *