Duru za habari zimeripoti hivi karibuni kwamba, wanajeshi wa muqawama wa Palestina walifanya oparesheni 22 dhidi ya Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan katika muda wa saa 24 zilizopita.
Kituo cha Takwimu na Habari cha Palestina kinachojulikana kwa jina la “Mu’ti” kilitangaza kuwa, vikosi vya muqawama vya Palestina vilifanya operesheni 22 dhidi ya Wazayuni wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wa muqawama wa Palestina walikabiliana na wanajeshi wa Kizayuni kwa kuwafyatulia risasi na kuwarushia vifurushi vya vilipuzi katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Jerusalem inayokaliwa kwa mabavu.
Ripoti hii inaongeza kuwa operesheni za vikosi vya upinzani zilifanyika katika maeneo ya Salafit, Qalqilya, Jenin, Bethlehem, Hebron, Ramallah, Nablus na Tulkarem, na vikosi hivyo vya upinzani vilikabiliana na kuwashambulia Wazayuni.
Kwa mujibu wa ripoti hii, vikosi vya upinzani vilishambulia makazi ya Wazayuni ya “Haramish” yaliyoko kaskazini mwa Tulkarm na kulenga basi lililokuwa limebeba walowezi huko Beit Amr iliyoko kaskazini mwa Hebroni.
Mashambulizi ya vikosi vya muqawama yalifanyika huku wanajeshi wa Kizayuni wakiwauwa Wapalestina wanne kwa kumshambulia Jenin siku ya Alhamisi.
Vikosi vya Al-Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya Hamas, lilijibu shambulio hilo na kutangaza kwamba, ikiwa utawala wa Kizayuni unadhani kwamba mashambulizi hayo yatasababisha kuvurugika azma ya muqawama wa Palestina, basi ni makosa makubwa.
Hapo awali Kituo cha Mu’ti kiliripoti kuwa mwezi uliopita vikosi vya muqawama vya Palestina vilifanya oparesheni 1,177 dhidi ya Wazayuni wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuikalia kwa mabavu Jerusalem na kusababisha vifo vya Wazayuni wanane na kujeruhiwa askari na walowezi 43.
Hali za siku hizi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu hususan katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni makhsusi mno, na wapiganaji wa Palestina wanajibu jinai zisizo na idadi za Wazayuni kwa njia yoyote ile, na jambo hilo limeweka mazingira maalum kwa Wazayuni watekaji nyara.
Kabla ya hapo, Wazayuni walipigana tu na Wapalestina wa kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na katika eneo la Ghaza, lakini hivi sasa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ulioko mashariki mwa Palestina umekuwa maficho ya Wazayuni waoga kutokana na vikosi vya kijeshi vya vijana wake. na imewanyima usingizi mnono.