Mwaka wa 2021 unapokaribia kuisha, jumuiya ya kimataifa inakabiliwa na majanga kadhaa ya kibinadamu na yale ya usalama yanayoibuka kila uchao, hata zaidi ya janga la kimataifa ambalo limeikumba dunia kwa miaka miwili.
Ethiopia inakumbwa na vita tata vya ndani ya nchi baina yao wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha maafa ya kiasi kikubwa ya kibinadamu, huku karibu watu milioni moja sasa wakiishi katika mazingira yasiyoridhisha, janga la njaa likiwa moja kati ya matatizo makuu katika nchi hiyo. Wakati huo huo, Urusi imekuwa ikijenga uwepo wake wa kijeshi kwenye mpaka wake na nchi ya Ukrania, na kuongezeka kwa mvutano baina yake na nchi za Kimagharibi na kuzua hofu kwamba kutakuwa na shambulio jingine dhidi ya mamlaka ya Ukrania. Na ndani ya nchi ya Afghanistan iliyochini ya umiliki wa Taliban, watoto wengi wanatarajiwa kufa msimu huu wenye baridi kali kutokana na njaa ikilinganishwa na jumla ya raia waliouawa katika miongo miwili iliyopita ya vita.
Migogoro hii inatofautiana , lakini marekani imetoa jibu kwa pande zote husika kwa kutumia zana za kisiasa, ambazo ni; vikwazo vya kiuchumi. Kwa upande wa Ethiopia, Rais Joe Biden ametishia kuwawekea vikwazo wanachama wa pande zote mbili za mzozo, pasi na kutathmini uwepo wa athari kubwa katika pande zote mbili.