Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi ya kuvuka mipaka yote ya dhulma – Viongozi wa nchi za Kiislamu walifanya makosa katika mkutano wa OIC kwa kuwapa Israel ruhusa ya kuvuka mipaka

Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

(Mkuu wa shule Jamia Urwatul Wuthqa – Lahore)

Imetolewa katika msikiti wa: Masjid Baitul ul Ateeq

Lahore – Pakistan

November 17, 2023

 

Hotuba ya 1: Viongozi wa nchi za Kiislamu walifanya “Haram” katika mkutano wa OIC kwa kuwapa Israel ruhusa ya kuvuka mipaka yote ya dhulma.

Inawezekana tukamwona mtu kama ndugu lakini kiuhalisia, akawa ni  adui na vile vile kinyume chake. Je tabia zetu zinaonyesha ubinadamu au la. Tunapaswa kuangalia ndani ya nafsi zetu wenyewe na kuona ni kiasi gani tumejitenga na ubinadamu. Kama ilivyo kwa Imam Ali (a), nyuso zao ni kama wanadamu, ila roho zao ni za kinyama na za kishetani. Tunapotazama upeo mkubwa katika jamii nyingine duniani tunaweza kutambua ni jinsi ubinadamu umesalia ndani yao. Msingi wa dini upo kwenye Taqwa na msisitizo wa Taqwa katika sheria ni zaidi ya ibada kwakua huo ndio msingi wa maisha.

Tutakapoitathmini Taqwa katika watu wa dini basi inabidi iwe chaanzo cha ulinzi wa ubinadamu, kwa hivyo angalia tu ni  jinsi gani ubinadamu unavyoonekana katika sehemu ya kidini. Wale walio na dini wanaomuamini Mwenyezi Mungu, na kuamini vitabu vya Mwenyezi Mungu, na Mitume wake pamoja na sheria za Mwenyezi Mungu, utagundua ya kwamba ndani yao mna wa kiasi kizuri cha ubinadamu. Baadhi utawaona wakiabudu ipasavyo na kutoa matambiko kwa mapenzi ya hali ya juu lakini ndani yao hamna ubinadamu hata kwa kiasi kidogo. Mtu aliye na dini anapokuwa adui wa mwenzake aliye na dini na kisha uadui huu ukafikia kua chuki, na mauaji basi tunaweza kusema kuwa wamejifunza dini pasi na kutekeleza Taqwa. Asiyekuwa na dini anamiliki mafuta lakini mwenye dini anatumia vyanzo vyake vyote vya kidini, na elimu yake kama njia ya kuwaua wanadamu wenzake,  jambo ambalo linahesabika ya kuwa ni kitendo kitakatifu kinachompa mtu Jannah. Tuseme tunawaona watu wote wa kidini wenye msimamo mkali, dini yao imeonyesha msimamo wao mkali na matokeo yake, dini hii bila Taqwa haitakua na misingi yeyote na ni sawa na kutokuwepo. Historia ni shahidi kama hivyo na tukishuhudia karibu nasi tunaweza kuona kinachoendelea. Lakini hatuamini katika kushuhudia kwetu badala yake tu kufuata yale ambayo wengine wanasema. Hii ina maana kwamba tunafunga macho yetu na kufungua masikio yetu. Tunapaswa kufungua macho ili tuishi katika hali ya sahii.

Ikiwa Quran ni silabasi ya dini hii, basi kila aya inatakiwa mwisho wake ukome kwenye Taqwa, lakini katika mtaala wa dini yetu, hakuna Taqwa iliyotajwa kabisa. Nimemtaja Allama Tabatabai (ra) ambaye amesema katika juzuu ya 6 ya Tafsirul Mizan kwamba; inasikitisha kuona kwamba mfumo wetu wa ufundishaji wa seminari ya kidini unakwenda bila hata ya kufungua ukurasa mmoja wa Quran katika muda wote wa masomo, na hili linnaweza wafanya wanafunzi kuwa Mujtahidin wakubwa. Huu ni ukweli ambao ameueleza kwamba bila ya Quran watu wanaweza kuwa Mufti na bila Quran Fatwa zao zingekuwa za chuki na chuki.

Leo ni mtihani kwa ubinadamu wote ambapo hali hii ya kusikitishwa na ya aibu inaonekana huko Gaza. Israel na Amerika wanatekeleza unyama na hili ndilo linalotarajiwa kutoka kwao. Lakini wale wanaojiona kuwa watu wa dini. Gaza imeondoa pazia kutoka kwa wale wanaojiita Waislamu, ambao watu waliwaona kuwa watu wa kidini sana kutokana na madai yao. Ni kama tu huko Karbala vifuniko viliondolewa kwenye nyuso zao. Yazid alikuwa fisadi na kila mtu alimchukulia kuwa ni fisadi, mtu muovu akiwemo Banu Umayyah na Ubaidullah aliuliza ni vipi Yazid alifanywa kuwa mtawala wa dola wakati alikuwa mtu fisadi kiasi hicho. Wakati Mu’awiyah alipoamua kumfanya Yazid mrithi wake, alituma ujumbe wa wanachuoni hasa kuchukua maoni ya watu na kuangalia kama kuna mtu hatasimama dhidi yangu. Katika hali hii, walio wengi walijibu kuwa yeye ni mtu mbaya na fisadi waziwazi, hakuna wa kumkubali na uamuzi huo uangaliwe upya. Msomi mmoja wa Banu Umayyah aliwaambia Bani Umayya kwamba usiseme haya mengine yote Mu’awiyah atakuuwa. Waliuliza nini kifanyike basi. Alisema badala ya kumwambia Muawiya nenda kamwambie Yazid abadili tabia yake na aonyeshe kiasi fulani katika tabia yake ili watu wamkubali. Banu Umayyah walifanya mafunzo ya kisiasa kwa kuleta wataalamu kutoka ndani ya Banu Umayyah. Walimzoeza ni nini alichopaswa kufanya kwa uwazi na ni matendo gani maovu aliyopaswa kufanya ndani. Makusudio ya kutaja ni kwamba Imamu Husein hakumfunua Yazid kwa sababu tayari alikuwa ni mpotovu na mtu muovu aliyewekwa alama na kila mtu. Imamu Husein (a) alizifunua nyuso za Umma wa Kiislamu, wale watu wa dini ambao walikuwa wamejijengea umaarufu wa uongo.

 

Leo ni hali hiyo hiyo, ambapo hakuna utaji kwenye nyuso za Israeli, Amerika, Uingereza, na Ulaya. Wote ni wachafu, wachafu, wakandamizaji waovu ambao wamefanya ukandamizaji wa wazi. Watu waliojifunika pazia walikuwa ulimwengu wa Kiislamu. Israel imefanya uonevu wa kikatili zaidi ambapo wameingia Hospitali na kutesa wagonjwa, na madaktari. Wiki iliyopita siku ya Jumamosi kulikuwa na mkutano wa OIC Mjini Riyadh ambapo wakuu wa nchi zote za Kiislamu walikutana. Walithibitisha tu unyenyekevu na fedheha yao katika mkutano huo. Nchi chache zilitoa mapendekezo mazuri kama vile Iran, Uturuki, na hata Wawakilishi wa Pakistani waliunga mkono mapendekezo mazuri na wakazungumza kwa niaba ya Wapalestina. Nchi fulani zilitoa mapendekezo ya kuchukua hatua madhubuti. Kulikuwa na wingu la kishetani kwenye mkutano huo na hawakuweza hata kutoa taarifa ya kulaani. Mwishowe, kauli ya nchi 58 kuwa na nguvu za nyuklia, na vituo vya mafuta ilikuwa kwamba UN inapaswa kuchukua hatua fulani. Kabla ya hapo, Israel hawakuwa na ujasiri wa kuingia ndani ya Hospitali na kuwadhibiti lakini baada ya mkutano huu, waliingia ndani ya Hospitali hiyo na kuwapiga risasi wagonjwa kitandani, kuwafanya mateka na kuharibu Hospitali hiyo. Ulimwengu unajua kwamba mkutano huu ulitoa ishara kwa Israeli na kuwafanya waridhike kwamba wanaweza kwenda kwa kiwango chochote cha ukandamizaji na dola za Kiislamu hazitaonyesha hisia yoyote. Kisha Imamu e Kaaba akatoa khutba ya Ijumaa iliyopita ambapo aliwaonya Waislamu kuchukua hatua zozote dhidi ya Israel, mnapaswa kuitazama serikali yenu na kuwiana na maamuzi yenu ya dola. Simu hii inatoka Kaaba! Na kisha wakuu wa serikali huketi katika mkutano uliolaaniwa na wanawapa Israeli ishara kunufaika na fursa hiyo na kufanya utakaso. Kuna wengine wanatoa kauli nzuri kama Erdogan lakini hakuna anayechukua hatua yoyote. Bado ana uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara na Israeli. Wiki iliyopita Al Jazeera iliwasilisha kwamba hata leo biashara ya dola bilioni 8 inaendelea na Israeli. Hakuvunja makubaliano yoyote na Israeli lakini alitoa tu mazungumzo ya filamu. Je, ukweli ni upi ndani ya mazungumzo haya? Uturuki iliwasilisha pendekezo hili la kusitisha uhusiano wa kidiplomasia kupitia Balozi na Israel ambao ulikuwa kabla ya mkutano huu ulioelezwa na Imam Khamenei (d.a). Hapa pendekezo hili lilikataliwa huku waliotangulia wakiwa UAE na Bahrain wakisisitiza kutofanya hivi. Haya yote yaliamuliwa kabla na rasmi walisema hatuwezi kuvunja uhusiano na Israeli. Mkutano huu ulikuwa wa watu wa fedheha zaidi ambao ulitoa ujasiri zaidi kwa Israeli na umefikia kikomo cha mwisho. Waislamu hawa hawana ubinadamu ndani yao.

Baada ya watawala, ngazi inayofuata ni ya wasomi wa kidini. Kuna wakuu wa nchi 58 lakini wasomi ni mamilioni katika ulimwengu wa Kiislamu. Wao ni wa kila madhehebu. Tukiwapima wanavyuoni hawa mtawala alikuwa mmoja na baadhi ya magavana, lakini wanachuoni walikuwa wengi, basi ni nini jukumu lao wakati wa Karbala hata baada ya Karbala walinyamaza kimya. Imamu Husein (a) aliitisha mkutano mkubwa wa Maulamaa huko Mina wakati wa Hijja mwaka mmoja kabla ya Karbala. Amefahamisha kuwa heshima yote waliyoipata wanazuoni inatokana na dini. Watawala wanaweza kuingia madarakani na kupata heshima kwa nguvu, lakini wanazuoni, wana dini na Uislamu tu. Ni katika historia kwamba masahaba walipohama kutoka Makka wangekuwa na kipande kimoja cha Tarehe cha kushiriki miongoni mwao kwa kulamba tu. Lakini masahaba hao hao walipoondoka duniani walikuwa na mali kubwa. Haya yote yalikuja kwa jina la Uislamu. Heshima, hadhi na heshima vyote vilitokana na Uislamu. Leo wanachuoni wanaheshimika kutokana na Uislamu, wana elimu, wamesoma Uislamu, na watu walioongoka. Imamu Husein (a) alitukumbusha kwamba heshima yote uliyo nayo inatokana na dini. Jukumu moja kubwa la Maulamaa ni kuwaunga mkono wanaodhulumiwa na kusimama dhidi ya madhalimu. Angalau kuwaongoza watu. Wote wanasikiliza na kuangalia matukio. Matukio haya ni ya kusikitisha sana hivi kwamba siwezi hata kuyatazama. Mpaka leo ndani ya siku 41, tumefanya nini na mashambulizi ya kuendelea? Je, utasubiri kiasi gani? Hii ni ishara kwamba wanataka kuharibu mbio za Wapalestina kutoka kwa ulimwengu. Wale wasomi ambao wanaendelea kupaza sauti zao ni wa kipekee lakini wengine ambao ni mamilioni ya kile wanachofanya. Wanazuoni wote wakikusanyika sehemu moja wanaweza kuwa zaidi ya milioni 1 na kutoa kauli ya pamoja ukandamizaji huu unaweza kukoma. Watu wanawafuata wasomi hawa.

 

Kundi la tatu ni wanasiasa hasa hawa waliopo nchini Pakistani ambao wamezama katika tamaa na anasa ya maisha na mamlaka. Wanasiasa hawa ni sehemu ya watawala hawa. Wanasiasa hawakufanya mkusanyiko wowote. Hata kutoka Jamaat e Islami, wakuu wao wa kisiasa hawakuja. Huko mjini Mansoura, walifanya mkusanyiko ambapo mimi nilikua mingoni mwa walioitwa. Nilimuuliza naibu chifu wao wako wapi wale wasomi 200 walioahidi Lahore kupaza sauti zao. Hakuja msomi hata mmoja. Wanasiasa wanashughulika kusambaza viti na madaraka yao. Maulamaa wa kimadhehebu wanaonyesha chuki kubwa dhidi ya Mashia lakini vipi sasa? Wanachuoni hawa wameiharibu akhera yao. Watalazimika kuomba msamaha na kukubaliwa matendo yao kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wanapaswa kufanya toba kwa siku 41 ili waweze kukubaliwa msamaha wao. Watu wanafuata Wanachuoni na madai yote ya Quran na Sunnah ni ya uwongo. Wanakubali wanachosema wanavyuoni hawa. Makundi haya matatu yameufanya ulimwengu wa Kiislamu kufikia hali hii ya fedheha. Karbala ya Gaza wamefunua nyuso zao. Wanasikiliza vilevile kwamba kwa muda wa siku 40 wanawake na watoto wangali wamefukiwa chini ya vifusi vya majengo yaliyolipuliwa. Na watu wangali wanawafuata tu. Katika kupaza sauti zao dhidi ya haya wanaweza kusababisha tofauti katika baadhi ya mambo. Hii inamaanisha kuwa hautoki Gaza lakini unaonyesha ni jinsi gani unashirikiana nao katika yale wanayo yapitia. Angalau tukipaza sauti yenye matokeo. Shinikizo huenda lisiwafikie. Tunahitaji kulifanya hili katika njia ya ufanisi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape afueni hawa wanaodhulumiwa katika janga hili la vita.

 

Hotuba ya 2: Maandamano ya Machi 19 ni wajibu kwa kila mmoja wetu ambapo hatua inayofuata itatangazwa.

Leo hii uchunguzi huu mkali wa Mwenyezi Mungu upo mahali ambapo ubinadamu wote unahusika katika hili. Mwenyezi Mungu anafanya mchujo na amewabainisha wale ambao ni waumini kwa majina tu, lakini kiuhakika wao ni wanyama; umewabainishia jinsi ambavyo Qur’an inavyosema; ya kuwa viziwi, mabubu na vipofu ni wale ambao Mwenyezi Mungu anachukia na kama isemavyo Quran kuwa ni mbaya zaidi miongoni mwa viumbe vitambaavyo ardhini. Hawasemi, hawasikii, wala hawaoni, leo hii tunaweza kuona hawa ni akina nani. Leo ambao hawasemi, wasione uonevu. Huu ni uchunguzi wa ubinadamu wote na sio wa Wapalestina pekee. Kila mtu amefichuliwa na wote wamekuwa uchi mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa siku 40 ukandamizaji umekuwa ukiendelea katika kila siku. Hawaonyeshi mwitikio wowote. Sio wasomi wala watawala, na hata wanasiasa hawakuchukua hatua yoyote. Jamii moja ambayo inaweza kufanya kitu ni raia wa kawaida. Wasomi wamejitokeza kama wahalifu. Watu wanaweza kuokoa heshima yao mbele ya Mwenyezi Mungu na wanaweza kuokoa nyuso zao. Kama ilivyosemwa hatuamini tunachoshuhudia bali tunaamini kile tunachokisikia.

Imamu Husein (a) alituma mabalozi sehemu mbalimbali,  wawili kati yao kuelekea mjini Basra kama vile vikundi viwili vya Shia ambavyo havikuwa na maelewano mazuri kati yao. Wakati huo balozi mmoja aliofikia aliuawa kishahidi na Ubaidullah. Balozi wa pili alikwenda kwa kundi jingine, na alikuwa chifu wa makabila madogo. Aliwaita viongozi wa makabila madogo na kuwaambia kwamba hii ndiyo barua iliyoandikwa na Imamu Husein (a) mwenyewe akiomba msaada, basi ni nini ushauri wenu, tufanye nini? Je, tumuunge mkono Imamu, Banu Umayyah au tusiwe na wasiwasi? Viongozi wa makabila madogo, ambao majina yao yametajwa katika historia walisimama mmoja baada ya mwingine na kusema jambo moja wewe ni kiongozi wetu chochote utakachoamua tutafanya, tuko tayari kutoa maisha yetu kwa ajili yako. Hali hiyo hiyo iko leo. Watu hawaangalii Dini, Quran, Allah, na Imamu Husein (a). Katika mkusanyiko huo, hakuna aliyesema chochote ambacho ni amri ya Mwenyezi Mungu tutaifanya, au Imamu Husein (a) ni Imamu wetu hivyo tutamsaidia. Leo ni hali hiyo hiyo. Shia wafanye nini kwa Gaza? Quran, Mtume, Imam anasema nini? Nini kingekuwa kisimamo cha Mtume (s), Imam Ali (a) na Imamu Husein (a) kama wangekuwepo leo? Ikiwa wewe ni Shia na unaijua tabia ya Imamu wako basi unapaswa kujua wangefanya nini basi nawe ufanye vivyo hivyo. Ikiwa ukiwa Mwislamu hujui hata Mtume (s) angefanya nini basi wewe si Mwislamu. Je, hakuna anayejua fatwa ya Mtume, Ahlulbayt (a)? Nitasimulia Fatwa ya Mtume na Ahlulbayt, kisha baada ya haya, unakwenda popote unapotaka kwenda, unaweza kwenda na ungehesabiwa pamoja nao tu. Imamu Husein (a) alisema katika safari yake kwamba utalelewa pamoja na Imamu wako unayemfuata hapa duniani. Wale wote wanaodhulumu, kuunga mkono madhalimu, na kukaa kimya wote ni sawa.

Katika kitabu Wasaelu Shia, Sura ya Amr na Nahy katika mada ya “Sura ya Wajibu wa kupanga mambo ya Waislamu”. Ukitaka kujua Fatwa ya Marehemu Hurr al-Ameli basi kichwa cha somo cha sura hiyo kinasimulia hukumu yake. Aliona  kuwa ni wajibu kwake kusimama na Umma wa Kiislamu na sio familia yake.

Imamu Sadiq (a) anasema: Asiyezingatia mambo ya Waislamu si Mwislamu.

Anaweza kuwa anafanya ibada, anatekeleza Hajj lakini hawi sehemu ya matatizo na maumivu ya Waislamu wenzake, basi yeye si Muislamu.

Mtume Muhammad (saww): Mwenye kuanza siku yake hadi siku ikapita na akawa hafanyi mpango wowote kwa ajili ya mambo ya Waislamu basi yeye si Muislamu.

Hili ni jukumu la kila siku.

Imamu Sadiq (a): Mtukufu Mtume (saww) anasema kwamba mtu anayeanza siku na asishiriki katika mambo ya Waislamu hatahesabiwa miongoni mwa Waislamu. Na mwenye kusikiliza maombi ya mtu yeyote (hata kama si Muislamu), akiwalingania Waislamu na asiitikie basi yeye si Muislamu.

Katika kumbukumbu za Mtukufu Mtume (s) yeye si Mwislamu ingawa anaweza kuwa anadai kuwa yeye ni Mwislamu. Kama ambavyo katika Quran, imetajwa baadhi ya watu wanaodai kuwa sisi ni waumini, lakini Mwenyezi Mungu akawajibu kuwa wao si waumini bali ni Waisilamu. Sisi ni Waislamu kwa sababu tumekula vyakula vingi kwa jina la Uislamu, tumefanya ibada, matambiko kwa hivyo tumekuwa Waislamu. Mtume anasema mtihani wako wa imani na kuwa Mwislamu ni pale mwenye kudhulumiwa anapowaita Waislamu kuomba msaada, Muislamu akipuuza basi si Muislamu. Huu ni wito wa Imamu wenu. Hata kama hadith hii haikuwepo, Karbala ilitutosha. Kuunga mkono dhulma, na kukaa kimya ni Haramu. Viongozi wa serikali walifanya Haram katika OIC kwa mujibu wa Quran, Mtume na Kitabu.

Ikiwa wewe ni miongoni mwa Waislamu, basi toa uthibitisho kwamba uko pamoja na Waislamu. Hawa Waislamu waoga kwa sababu ya kuiogopa Marekani hawapazi sauti zao, tunapaswa kuchukua hatua hiyo kwa njia ya ufanisi kiasi kwamba wengine watasisimka. Kuinua bendera yako kwa shirika lako sio kupaza sauti kwa waliodhulumiwa.

Ulimwengu unaweza kuona na ni katika rekodi ambazo tumekuwa tukifanya na tunaweza kufanya makongamano, programu kubwa, na mikutano ya hadhara peke yetu. Lakini tumetoa upendeleo kujiunga na Waislamu wengine ili iwe na ufanisi zaidi na kuipa ulimwengu taswira hii ya kivitendo kwamba Masunni wa Shia wameungana katika suala la Gaza. Ili kutoa ujumbe kwa wakandamizaji, kuna mkutano wa hadhara tarehe 19. Mikutano hiyo haitoshi, leteni watu kwenye mikutano na wapeni hatua inayofuata. Baada ya kila mkusanyiko, kunapaswa kuwa na hatua inayofuata ambayo pia pamoja na wengine. Ikiwa ningelazimika kuifanya peke yangu ningetangaza ni hatua gani inapaswa kuwa inayofuata. Watu wa Pakistani ni waumini, wako tayari kuchukua hatua yoyote. Faida zisizo sahihi zimechukuliwa na wanasiasa kwa kuinua hisia zao. Ikiwa utauawa mahali pengine baadaye kwa kutokwenda Karbala basi hakuna faida yoyote. Inatubidi kuwa sehemu ya Karbala inapotokea na sio kuchelewa. Umma mzima, huko Lahore, na kuzunguka miji inapaswa kuanza kampeni ya mwaliko katika siku mbili, na tarehe 19 Novemba, Waislamu wa Lahore wangepaza sauti zenye matokeo kwa ndugu zao huko Gaza. Hii ndiyo fatwa na kauli ya Mtume (saww) ambayo hakuna thamani ya Mufti yeyote. Mtume anasema ikiwa mtu yeyote anaomba msaada, basi usione dini yake inaitikia tu. Quran inasema wakiitwa watoto na wanawake hiyo inatupa wokovu kutoka kwa madhalimu hawa. Ewe Mwenyezi Mungu tuletee mlinzi. Ukiinuka kwa ajili ya hawa waliodhulumiwa basi umejithibitisha kuwa Walii na Nasir kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Wanawake pamoja na watoto waje pamoja na watoto wao wachanga mikononi ili kuonyesha ulimwengu ya kua tuko pamoja na hawa wanaodhulumiwa. Wakati wa kuinuka unapofika, basi acha nafasi zote za kukaa. Lahore nzima inapaswa kuwasilisha hali hii ya kwamba tuko pamoja na Gaza. Kisha tutawasilisha hatua inayofuata pamoja na wengine na hata ikiwa hawakubaliani, tutachukua hatua mwafaka. Wakati Karbala inaendelea, hatutaonyesha fedheha kama walivyofanya watu wa Kufa. Wakati Karbala inaendelea tunapaswa kuwa sehemu yake na kujihesabu kuwa miongoni mwa maswahaba waliotayari kuihami dini. Hatupaswi kuwa viziwi, au mabubu ili tufe kisha tuwe mateka. Miji yote karibu na Lahore itashiriki katika maandamano haya.

Mwenyezi Mungu atuonyeshe siku hiyo ambayo sote kwa pamoja tutakwenda katika Masjid al-Aqsa na kutoa uthibitisho wa kuwa Umma wa Kiislamu umesimama pamoja nao.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *