Mvua kubwa yaathiri mamia nchini DRC Congo, 300 wafariki dunia

Waziri Modeste Mutinga Mutuishayi  alitoa taarifa hiyo wakati wa mkutano wa kutathmini mgogoro huo wa kimaumbile na kuongeza kuwa, takriban nyumba 43,750 zimebomoka. Pia alionya juu ya hatari ya kuzuka majanga mengine mbalimbali ya kiafya kutokana na ukosefu wa vyoo na maji safi.

Waziri huyo ametoa wito kwa serikali ya Kongo kutoa fedha haraka za kuwasaidia waathiriwa wa mvuo hizo, huku akitoa wito pia wa mshikamano wa kimataifa wa kuzisaidia timu za misaada ya kibinadamu zinaendesha shughuli zao hivi sasa ndani ya maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi ni vitu vya kawaida huko DRC wakati wa msimu wa mvua, ambao unaanza Septemba hadi Mei.

Mwezi Mei mwaka jana takwimu zilizotolewa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zilisema kuwa idadi ya watu walioaga dunia kufuatia janga la mafuriko na maporomoko ya udongo mashariki mwa nchi hiyo ilifikia 438.

Takwimu hizo za maafa ya mafuriko DRC zilionyesha pia kuwa, watu wengi zaidi walipotea na idadi hiyo ya vifo vya watu 438 ni ndogo ikilinganishwa na idadi hasa ya maafa hayo.

Katika vijiji kadhaa vilivyoko karibu na fukwe za Ziwa Kivu, watu walikuwa wakichimba tope kwa mikono katika juhudi za kutafuta jamaa zao waliopotea.

Vyombo vya habari vya ndani ya DRC viliripoti kwamba katika moja ya vijiji vya Kivu Kusini zaidi ya robo tatu ya nyumba zilisombwa na maji ikiwa ni pamoja na vituo vya afya na skuli.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *