Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vilidai kwamba serikali ya Somalia inajaribu Kurekebisha mahusiano na utawala huo na kujaribu kuurudisha katika hali ya kawaida.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Fars, vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vilidai kuwa Mogadishu imeamua kuchunguza suala la kuhalalisha uhusiano na utawala wa Kizayuni.
Kulingana na msemaji wa Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud, mtandao wa Kizayuni wa Kan ulidai kuwa serikali ya Mogadishu itajadili suala la kurekebisha uhusiano na Tel Aviv na wabunge na vyama vingine.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kizayuni, msemaji wa rais wa Somalia alitoa kauli hizo akijibu swali kuhusu ripoti zinazohusiana na kuhalalisha uhusiano kati ya Somalia na utawala wa Kizayuni.
Ripoti ya gazeti la Russia Today imebainisha kua chombo hiki cha habari cha Kizayuni pia kilidai: “Hassan Sheikh Mahmoud, baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa nchi yake, wakati wa safari yake ya Imarati mwishoni mwa mwezi wa Mei uliopita, alikutana na maafisa wakuu wa Israel; ambayo ofisi ya Rais wa Somalia ilipinga swala hilo”.
Mwaka 2016, Hassan Sheikh Mahmoud alikutana na Benjamin Netanyahu aliyekua Waziri Mkuu wa wakati huo wa utawala wa Kizayuni.