Wabahraini waandamana kumuenzi Shahidi Ayatullah al Nimr

Wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano ikiwa ni katika kumbukumbu ya kumuenzi Shahidi Ayatullah Sheikh Nimr Baqi al Nimr kiongozi wa Waislamu wa Kishia wa Saudi Arabia aliyeuliwa shahidi na utawala wa Aal Saud.

Utawala wa Aal Saud tarehe Pili Januari 2016 ulimnyonga Sheikh Nimr Baqir al Nimr mwanazuoni mtajika wa Saudi Arabia baada ya kufungwa jela kwa miaka minne. Sheikh Nimr alinyongwa na utawala wa Aal Saud kutokana na hatua zake za kuukosoa utawala huo wa kifalme. Waislamu katika nchi mbalimbali walilaani vikali hatua ya Saudia ya kumnyonga Sheikh Nimr Baqir al Nimr. Wakazi wa kisiwa cha Setra na kitongoji cha Sanabs huko Bahrain wamefanya maandamano na kulaani kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya Manama na Tel Aviv na kuanza mwenendo wa mapatano kati ya Bahrain na utawala wa Kizayuni.

Waandamanaji wa Kibahraini walikuwa wamebeba picha za Shahidi Ayatullah Nimr Baqir al Nimr na kutangaza mshikamano wao na familia ya mwanazuoni huyo mtajika wa Saudi Arabia na watu wa nchi hiyo.

Bahrain na utawala haramu wa Kizayuni Septemba 15 mwaka 2020 zilisaini rasmi mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida kati ya pande mbili huko White House chini ya usimamizi wa Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump. Kuhuishwa uhusiano kati ya Bahrain na utawala wa Kizayuni kulikabiliwa na upinzani na ukosoaji mkubwa katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *