Wafuasi matajiri wa Marekani wa utawala wa Kizayuni wameanzisha kampeni katika mitandao ya kijamii, kwa lengo la kukusanya michango ya fedha kwa ajili ya kumuunga mkono “Don Samuels” na kukabiliana dhidi ya Ilhan Omar; Muislamu na mgombea mpinga wa Kizayuni katika uchaguzi wa awali wa Chama cha Demokrasia nchini humo katika jimbo la Minnesota.
Madhumuni ya kikundi hiki ni kuchangisha fedha kwa ajili ya Kamati ya Kisiasa na Mikakati ya Utekelezaji ili kumuunga mkono Samuels kama mwanachama wa Republican.
Alex Main, mshauri wa kampeni hiyo, alisema wanachama hao wana uwezo wa kumwangamiza Ilhan Omar, adui nambari 1 wa Wayahudi, Israel na Amerika.
Alisisitiza kuwa juhudi za kumshinda Ilhan katika uchaguzi ujao zinaendelea.
Hii si mara ya kwanza kwa majaribio ya kumuondoa Ilhan kwa sababu ya upinzani wake dhidi ya utawala wa Kizayuni.
Mapema mwaka huu, wabunge wengi wa chama cha Republican katika Baraza la Wawakilishi la Marekani walimuondoa Ilhan katika Kamati ya Masuala ya Afrika ya Bunge la Congress la Marekani kwa sababu ya misimamo yake dhidi ya Uzayuni.
Kamati ya Bunge ya Masuala ya Afrika ni tawi la Kamati ya Mambo ya Nje ya Baraza ambalo lina mamlaka juu ya masuala ya kidiplomasia na usalama wa kitaifa kama vile misaada ya kigeni, vita, na kuwekewa vikwazo vya kimataifa.
Tangu Warepublican wachukue udhibiti wa Baraza la Wawakilishi Novemba mwaka jana, McCarthy ameapa kufanya kazi ya kumwondoa Ilhan madarakani.
Akasema: Nakumbuka alivyosema Ilhan kuhusu Israel mwaka jana, tangu hapo niliahidi kwamba Ilhan hatakuwepo tena katika mambo ya nje na nitatimiza ahadi hii.
Ilhan Omar ni mwanasiasa Mwislamu wa Marekani mwenye asili ya Kisomali, ambaye alipata umaarufu baada ya kushinda Baraza la Wawakilishi la Jimbo la Minnesota kutoka Chama cha Kidemokrasia.
Omar aliikimbia nchi yake baada ya kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia mwaka 1991. Alikaa miaka 4 katika kambi ya wakimbizi nchini Kenya, kisha akahamia Amerika na familia yake mwaka wa 1995. Waliishi kwanza Arlington, Virginia, lakini wakahamia Minneapolis mwaka huo huo.