Wafungwa wa Ethiopia nchini Saudi Arabia wanalazimika kuchoma nywele zao

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limechapisha kipande cha video kinachoonyesha kuwa wafungwa wa Ethiopia nchini Saudi Arabia wanalazimika kunyoa nywele zao kwa kuzichoma moto kutokana na ukosefu wa vifaa vya usafi katika magereza hayo.

Kurasa za upinzani za Twitter zimenukuu shirika la Amnesty International likisema kuwa mamlaka ya Saudia haitoi sabuni au vifaa vingine vya kusafishia wafungwa hao, na kwamba wanaugua magonjwa ya ngozi kutokana na ukosefu wa usafi.

Wafungwa wawili wa zamani walisema: Nywele zetu zilipopata chawa, walitulazimisha kuchoma nywele zetu badala ya kuzikata.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *