Mgogoro wa gharama kubwa za maisha nchini Uingereza umekuwa sababu ya Waingereza katika baadhi ya miji kula chakula cha wanyama wa kufuga majumbani.
Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kwamba wananchi “wanakula chakula cha wanyama” kwa sababu hawawezi kumudu chakula cha kawaida.
Ripoti zinasema, baadhi ya maeneo ya Wales yamekumbwa na umaskini mkubwa kiasi kwamba watu wamelazimika kushuka hadi ngazi za chini ili kulisha familia zao tu.
Habari hii imekuja baada ya data mpya ya Sensa kuonesha kuwa baadhi ya jamii za watu maskini zaidi huko Wales ziko Cardiff, mji mkuu wa Wales.
Mwezi uliopita, gharama za chakula zilipanda tena, huku bei za bidhaa hiyo zikiwa asilimia 12 zaidi ya ile ya mwaka mmoja uliopita.
Mark Seed, ambaye anasimamia mradi wa chakula cha jamii huko Trowbridge mashariki mwa Cardiff, ameambia BBC kwamba: “Bado ninashtushwa na ukweli kwamba tuna watu wanaokula chakula cha wanyama.”
Takwimu rasmi za serikali zinaonyesha kuwa mfumuko wa bei nchini Uingereza ulipanda na kufikia kiwango cha juu zaidi ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu miaka 41.
Serikali ya Uingereza inaendelea kulaumu vita vya Ukraine na janga la COVID -19 kama sababu kuu za kuzorota kwa uchumi.