Wanaharakati wanawake 35 wa Saudia wahukumiwa kifungo cha miaka 11 jela

Vyanzo vya mashirika ya kutetea haki za binadamu vimeripoti kuwa wanaharakati wanawake 35 wa Saudi Arabia wamehukumiwa kifungo cha miaka 11 jela na utawala wa Al-Saud.

Haki za binadamu ni kitu kigeni kwa wananchi wa Saudia kwa sababu kwa muda mrefu wamenyimwa hata haki za kimsingi na hadi sasa pia hawajaweza kufaidika na haki za kisiasa kama inavyostahiki.
Kuhusiana na suala hilo na kwa mujibu wa televisheni ya Al-Alam; wanaharakati wanawake 35 wa Saudi Arabia ambao majina yao hayajatajwa wamehukumiwa kifungo cha jumla ya miaka 11 jela katika hukumu iliyotolewa kiuonevu dhidi yao.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, katika miaka ya karibuni utawala wa Aal-Saud umekithirisha kutoa hukumu za kidhalimu dhidi ya wanaharakati wanawake wa nchi hiyo.
Mwaka uliopita wa 2022, ulishuhudia jinai na uhalifu mkubwa zaidi kuwahi kufanywa katika historia ya Saudi Arabia kwa kutolewa hukumu nyingi za kifo katika kipindi cha karne moja.
Kitambo nyuma, shirika la kutetea haki za binadamu la Saudia lenye makao yake barani Ulaya lilithibitisha suala hilo katika ripoti yake ya kila mwaka kuhusu haki za binadamu na kutahadharisha juu ya kuendelea kukiukwa haki za binadamu nchini Saudi Arabia na kutokea uhalifu na jinai za kutisha zaidi katika mwaka huu wa 2023.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *