Operesheni ya ufyatuaji risasi katika eneo la Hawara kusini mwa Nablus katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ilisababisha kujeruhiwa kwa wanajeshi 2 wa Kizayuni.
Kwa mujibu wa ripoti, wanajeshi 2 wa Israel wamejeruhiwa katika operesheni ya ufyatuaji risasi hii leo (Jumamosi) katika eneo la Hawara kusini mwa Nablus lililoko katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Katika muktadha huu, Idhaa ya Kiebrania 14 iliripoti kuwa wanajeshi 2 walijeruhiwa katika shambulio hilo la ufyatuaji risasi katika mji wa Hawara uliopo kusini mwa Nablus.
Gazeti la Jerusalem Post liliandika: Risasi hio ilifyatuliwa kutoka ndani ya gari lililokuwa likitembea na jeshi la Israel na kujaribu kuwakamata wahusika.
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa hali ya mmoja wa askari wawili wa utawala huo waliojeruhiwa kwa kupigwa risasi ni mbaya.
Vyombo vya habari vya Kiebrania viliripoti kwamba kufuatia tukio hili, askari wa utawala huu walitumwa kwa haraka ile kwenda katika eneo la tukio na kuzuia vivuko vya mji wa Nablus.