Wanajeshi 20 wa jeshi la kigaidi la Israel waangamizwa al-Shujaiya Gaza

Jeshl la kigaidi la Israel limekiri kuwa, wanajeshi wake 20 wameuawa katika kipindi cha wiki moja iliyopita katika mapigano kati yao na vikosi vya muqawama wa Palestina katika eneo la al-Shujaiya katika Ukanda wa Gaza.

Kamanda wa zamani wa brigedi ya “Golani” ya utawala wa Kizayuni amesema: Kikosi hiki kilipoteza robo ya vikosi vyake vya kijeshi katika vita vya Gaza.

Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni, amekiri kuwa wakati huu wa vita vikali kati ya wapiganaji wa muqawama wa Palestina na askari wa jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza, kuna mapigano makali katika Ukanda wa Gaza.

Ameongeza kusema kuwa, lengo letu la kuiangamiza HAMAS na kuwakomboa mateka liko thabiti na hatuna chaguo jingine.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, makumi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameangamizwa katika operesheni ya Brigedi za Izzuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu HAMAS.

Wakati huo huo, Abu Obeidah, Msemaji wa Brigedi za Al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amebainisha kuwa, vikosi vya adui vinakaribia kusambaratika na kuongeza kwamba, takwimu ambazo adui amezitangaza rasmi kuhusu vifo na majeruhi wake si za kweli.

Makundi ya muqawama ya Palestina yalianzisha operesheni ya kushtukiza ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Gaza (kusini mwa Palestina) dhidi ya maeneo ya utawala unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu mnamo Oktoba 7, 2023, na utawala huo kuanzisha mashambulizi ya kinyama katika Ukanda wa Gaza ili kulipiza kisasi, kufidia kushindwa kwake na kusimamisha harakati za makundi ya Kipalestina, kwa kufunga vivuko vyote vya eneo hilo na kulilipua kwa mabomu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *