Wanajeshi wa Israel wawashambilia waumini wa Kipalestina huko al-Quds, Ramadhani 2

Vikosi vya utawala wa Israel vimewashambulia Wapalestina katika Lango la Damascus huko al-Quds inayokaliwa kwa mabavu na kuwapiga vikali waumini wa Kipalestina na kuwatia mbaroni wengine katika usiku wa pili wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Ni jambo la kawaida kwa vikosi vya Israel kuzidisha  ghasia dhidi ya Wapalestina wanaokusanyika katika eneo hilo wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Siku ya Jumamosi, polisi wa Israel waliwatia mbaroni Wapalestina wanne katika usiku uliojaa ghasia na mvutano katika mji mkongwe wa al-Quds.

Vikosi vya utawala haramu wa Israel vilitumia ukatili na ukandamizaji siku ya Jumapili, kurusha maguruneti na gesi ya kutoa machozi dhidi ya Wapalestina na kuwapiga vikali waumini waliokuwa wakirejea kutoka kwenye swala ya jioni kwenye uwanja wa Msikiti wa al-Aqsa.

Takriban Wapalestina 20 walijeruhiwa katika mapigano hayo na wengine 10 kukamatwa na maafisa waliovalia mavazi ya kiraia ambao walijipenyeza kwenye umati wa watu.

Mapema asubuhi, makumi ya walowezi haramu wa Kiyahudi, wakisindikizwa na wanajeshi wa Israel, walivamia Msikiti wa al-Aqsa huko Quds inayokaliwa kwa mabavu. Haya yanajiri huku polisi wa Israel wakiweka vizuizi vya kutembea kwa waumini wa Kiislamu kwenye milango ya msikiti huo katika siku ya pili ya mfungo wa Ramadhani.

Hali ya wasiwasi inazidi kutanda katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu baada ya wanajeshi wa Israel kuwaua kwa kuwapiga risasi Wapalestina watatu katika Ukingo wa Magharibi wa mji wa Jenin siku ya Jumamosi.

Brigedi ya Al-Quds, tawi la kijeshi la Islamic Jihad imesema waliouawa ni wanachama wake, ikiwataja kuwa ni Saeb Abhera, 30, Khalil Tawalbeh, 24, na Seif Abu Libdeh, 25.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *