Wananchi wa Argentina waandamana kuliunga mkono taifa la Palestina

Makumi ya wananchi wa Argentina wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Buenos Aires na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa taifa madhulumu la Palestina.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba bendera za Palestina wakiwa pia na mabango na maberamu  yaliyoandikwa jumbe mbalimbali za kuwaunga mkono Wapalestina walikusanyika mbele ya ubalozi wa Israel mjini Buenos Aires na kupiga nara za kuulaani utawala huo ghasibu.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, waandamanaji hao walisikika wakipiga nara za kutangaza kuwa pamoja na taifa la Palestina na wakati huo huo kulaani siasa za kivamizi za utawala dhalimu wa Israel.

Waandamanaji hao waliokuwa na hasira kutokana na jinai na mauaji ya kila leo ya Israel dhidi ya wananchi wa Palestina wakiwemo watoto wadogo wasio na hatia wameitaja Israel kama utawala wa Kifashisti na kutoa mwito wa kuchukuliwa hatua utawala huo.

Juan Carlos Giordano, Mbunge wa Bunge la Argentina kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha ‘Socialist Left’ aliyeshiriki katika maandamano hayo ameweka katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamiii wa twitter picha yake akiwa katika maandamano hayo ya kuwaunga mkono Wapalestina.

Maandamano ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani siasa za kibaguzi za utawala wa Kizayuni wa Israel yameendelea kushuhudiwa kila pembe ya dunia na kuzidi kuonyesha kufeli sera za kibaguzi za Israel na waungaji mkono wake.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *