Wanawake Afghanistan wapigwa marufuku kwenda safari ndefu bila wanaume

Maagizo hayo yametolewa siku ya Jumapili chini ya utawala wa Taliban ambapo shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights limesema marufuku hiyo inawafanya wanawake kujihisi kama wafungwa.

Taliban imesema wanawake wa Afghanistan wanaotaka kusafiri umbali mrefu kwa barabara wanapaswa kupatiwa usafiri ikiwa tu wataandamana na ndugu zao wa kiume.
.

Maagizo hayo, yametolewa siku ya Jumapili, ikiwa ni marufuku ya hivi karibuni katika haki za wanawake tangu kundi hilo kuchukua madaraka mwezi Agosti.
.

Agizo hilo linasema wanawake wanaosafiri kwa zaidi ya maili 45 (72km) wanapaswa kusindikizwa na mwanafamilia wa karibu wa kiume.
.

Tangu Taliban ichukue mamlaka baada ya kuondoka kwa majeshi ya Marekani na washirika wake, mamlaka hayo yawamewaambia wafanyakazi wengi wa kike kubaki nyumbani wakati shule za sekondari zikiwa zimefunguliwa kwa ajili ya wavulana na walimu wa kiume pekee.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *