Wanunuzi wa pamba kutaifishwa mizani kwa watakaofanya udanganyifu

Bariadi. Katibu wa chama cha wanunuzi wa zao la pamba nchini, Boaz Ogola amebariki maamuzi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ya kuitaifisha mizani itakayofanya udanganyifu katika ununuzi wa pamba msimu huu.

Ogola ameyasema hayo leo Juni 30, 2022 katika mahojiano na waandishi wa habari ambapo ameelezea hatua hiyo  kuwa inalenga kuboresha maslahi ya mkulima na kuongeza tija hivyo ni wajibu wa serikali kulinda na kusimama haki za mkulima hivyo itaongeza uwajibikaji kwa wanunuzi na mkulima atanufaika.

Amesema wizi kupitia mizani kwa kipindi cha nyuma ulikuwa mkubwa ikilinganishwa na sasa ambapo matukio yamepungua na ambao bado wanaendelea na wizi huo hatua kali zichuliwe dhidi yao kwani kitendo hicho sio chema na ni kuminya haki ya mkulima.

“Kupanda kwa pamba siku hadi siku haimaanishi wanunuzi ni wengi, ni kwamba kuna uzarendo ndani yake, inawezekana soko la kimataifa likapanda lakini kama hakuna uzalendo bei haiwezi kupanda hivyo uzarendo ni pamoja na kuhakikisha mkulima wetu ananufaika zaidi,” amesema Ogola.

June 28, 2020 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila aliawaagiza maofisa wanaokagua mizani ya ununuzi wa pamba kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuikamata na kuitaifisha mizani iliyoharibiwa inayotumiwa na mawakala wasio waaminifu katika baadhi ya vituo vya ununuzi wa pamba mkoani.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Kafulila kubaini kuwa sheria ya faini ya Sh2 milioni kwa anayedhulumu kupitia mzani ni ndogo na haimuumizi mtenda kosa hivyo alimuelekeza RPC na maofisa wanaohakiki mizani kuhakikisha kwamba yeyote ataekutwa anaibia wakulima kwa kutumia mzani kwanza atalipa Sh2 milioni kama faini ya kisheria, atashikiliwa na polisi kwa saa 48 na mzani wake utashikiliwa mpaka baada ya msimu wa ununuzi wa pamba kwisha,” amesema Kafulila.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *