Kufuatia mashambulizi ya wanajeshi hao wa Kizayuni katika kambi ya “Aqaba Jabr” katika mji wa Erija, ulioko kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, mapigano yalizuka kati ya wapiganaji hao wa Kipalestina na askari wa jeshi la Kizayuni.
Duru za Palestina zimebainisha kuwa, wanajeshi hao wa Israel walishambulia kambi ya Aqaba Jabr na kuizingira nyumba ya “Maher Shelon” raia wa Palestina na kuwafyatulia risasi za kivita raia hao, na matokeo yake vijana watatu wa Kipalestina walijeruhiwa vibaya.
Mmoja wa vijana hao alipigwa risasi ya tumbo na hali yake ni mbaya. Vikosi vya uokoaji vilijaribu kuokoa maisha ya kijana huyu, lakini wanajeshi wa Israel walimkamata.
Jeshi la Israel pia liliwaweka kizuizini raia kadhaa na kuziba njia za kuingia kambi ya Aqaba al-Jabr, kuwazuia magari ya kubebea wagonjwa na waandishi wa habari kuingia katika kambi hiyo, na kumtumia raia wa Palestina na mtoto wake kama ngao za binadamu.
Kadhalika, Jumuiya ya Wafungwa wa Palestina imetangaza kuwatia mbaroni watu 6 katika hujuma ya leo ya wanajeshi wa Kizayuni kwenye kambi ya “Aqba Jabr” huko Yeriko.