Wapalestina 6 wapigwa risasi na kujeruhiwa katika ukatili mpya wa Wazayuni

Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewapiga risasi na kuwajeruhi Wapalestina sita wakati walipovamia maeneo tofauti ya Wapalestina hao katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Baraza jipya la mwaziri la Benjamin Netanyahu lilianza kazi rasmi tarehe 29 Disemba 2022. Wataalamu wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa, serikali hiyo mpya ya Israel ambayo imeundwa baada ya mkwamo mkubwa wa miaka wa mitano wa kisiasa, ndiyo serikali ya kifashisti zaidi na yenye misimamo mikali zaidi ya utawala pandikizi wa Kizayuni uliopachikwa jina bandia la Israel.

Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa, mapema leo Jumanne, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamevamia maeneo kadhaa ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwashambulia kwa risasi za kivita vijana wa Palestina.

Baadhi ya duru za kieneo zimetangaza kutokea mapigano baina ya vijana wa Palestina na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni katika eneo hilo ambapo vijana 6 wa Kipalestina wamejeruhiwa kwa risasi.

Duru mbalimbali za habari zinasema kuwa, wanajeshi wa israel wamemteka nyara Mpalestina mmoja aliyekuwa ameachiliwa huru kutoka kwenye jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni pamoja na baba yake katika eneo moja la Ramallah.

Wazayuni hawasiti hata kidogo kufanya jinai na ukatili wa aina yoyote ile dhidi ya Wapalestina katika njama zao za kufanikisha malengo yao haramu kwenye ardhi hizo wanazozikalia kwa mabavu kwa zaidi ya miaka 70 sasa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *