Wapalestina kadhaa watiwa mbaroni katika shambulio la Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan

Wanajeshi hao wa Kizayuni wanaoikalia kwa mabavu waliwatia mbaroni Wapalestina kadhaa kwa kushambulia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wanajeshi wa utawala huo ghasibu walivamia nyumba ya raia wa Palestina aitwaye Mohand Al-Kaabi katika kambi ya Askar al-Jadeed mashariki mwa Nablus na kumkamata.

Wazayuni hao pia waliwatia mbaroni raia kadhaa wa Palestina katika miji ya Nablus, Hebron, Ramallah na Jerusalem inayoikalia kwa mabavu.

Vikosi vya utawala ghasibu vya Kizayuni pia viliishambulia kambi ya Shuafat iliyoko mashariki mwa Jerusalem inayokaliwa kwa mabavu na kushambulia gari la Wapalestina na kumjeruhi dereva wake.

Dereva wa gari hilo alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi katika kambi hiyo, na ambulensi iliyokuwa imembeba kijana huyo aliyejeruhiwa ilinaswa kwenye lango la mji wa Anata kaskazini mashariki mwa Jerusalem.

Baada ya vikosi vya uvamizi kuvamia kambi hiyo, milio ya risasi nzito ilisikika.

Vikosi hivyo vilivyovamia kwa mabavu vile vile vilifunga kizuizi cha kambi ya Shuafat huko Quds kutoka kwa magari ya wakaazi kutoka pande zote mbili na kuzuia kuingia na kutoka kwenye makazi ya Anata kaskazini mashariki mwa Quds.

Shambulio hilo la askari wa Kizayuni katika kambi ya Shuafat lilifanyika kufuatia kifo cha mwanajeshi wa Israel katika operesheni dhidi ya Wazayuni katika kituo cha upekuzi cha Shuafat.

Vikosi hivyo vilivyovamia kwa mabavu vilevile vilivamia nyumba ya “Mohammed Bassel Zalbani”, ambaye kwa mujibu wa Wazayuni, alikuwa akijaribu kutekeleza operesheni kwenye kizuizi cha kambi ya Shuafat, na kuwakamata watu 4 wa familia yake baada ya kuharibu vifaa vya nyumbani.

Mlowezi wa Kizayuni pia alijeruhiwa katika shambulio la kisu katika eneo la kale la Jerusalem inayokaliwa kwa mabavu. Wakati huo huo, askari mmoja wa utawala huo ghasibu karibu na eneo la Shuafat Mashariki aliuawa katika operesheni ya kuchomwa kisu na Mpalestina, na kisha kupigwa risasi askari hao wanaoikalia kimabavu kupelekea kujeruhiwa askari huyo wa Kizayuni kwa milio ya risasi ya wananchi.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *