Wapiganaji wa Tigray wadai kuwateka nyara mamia ya wanajeshi wa serikali ya Ethiopia

Wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray (TPLF) ya kaskazini mwa Ethiopia wametangaza kuwa, wanawashikilia mamia ya wanajeshi wa serikali iliowateka nyara hivi karibuni.

Taarifa hiyo ambayo haikutoa maelezo zaidi imedai kwamba, hivi sasa mamia ya wanajeshi wa serikali wanashikiliwa na wapiganaji hao.

Kadhalika wanamgambo hao wamedai kuwa, wanajeshi wa Ethiopia wamekuwa wakiwatumia watoto wadogo kwa ajili ya kufikia malengo yao.

Madai hayo yanatolewa katika hali ambayo, kumekuweko na juhudi za kieneo na kimataifa zenye lengo la kuleta upatanishi baina ya pande mbili ili kuhitimisha vita hivyo ambavyo vinatishia kutokea maafa ya kibinadamu.

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, vikosi vya Ethiopia vikishirikiana na vya Eritrea vimeazisha mashambulio dhidi ya wapiganaji wa Tigray katika mji wa Adybayo.

Tangu mwezi Novemba mwaka juzi (2020) jimbo la Tigray limekumbwa na hitilafu na mivutano ya kisiasa kati ya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed na viongozi wa eneo hilo ambao wakati fulani waliongoza serikali ya Ethiopia.

Vita vilivyoshuhudiwa katika eneo hilo hadi sasa vimesababisha kuuliwa makumi ya maelfu ya watu na kupelekea mamilioni ya wengine kulazimika kuwa wakimbizi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP limessema kuwa hivi sasa watu milioni 22 barani Afrika wako kwenye hatari ya kupoteza maisha kutokana na baa la njaa.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *