Wapinzani wa Ufalme wa Uingereza waandamana katika jiji la London

Waingereza wanaopinga utawala wa Kifalme wameandamana hadi kwenye uwanja wa bunge katika mji mkuu wa nchi hiyo London.

Kwa mujibu wa televisheni ya Al-Mayadeen, waandamanaji hao wamekosoa vikali fedha zilizotumiwa na serikali kugharimia sherehe ya kutawazwa Mfalme Charles na kutaka kufutwa sheria inayopiga marufuku maandamano, ambayo polisi waliitumia kuwakamata wanaharakati wanaotaka mfumo wa Jamhuri siku alipotawazwa rasmi Charles kuwa mfalme wa nchi hiyo.
Mwandamanaji mmoja amesema: “tunataka Ufalme uondoshwe kwa sababu ni taasisi ya kale. Hatuna nia ya kufanya mapinduzi, lakini tunaamini ni wakati wa mabadiliko… Serikali inabeba gharama kubwa sana kwa ajili ya Ufalme. Sherehe ya kutawazwa iligharimu zaidi ya pauni milioni mia moja, na hiyo ni katika wakati ambapo raia wa Uingereza wanakabiliwa na hali ngumu sana ya maisha”.
Kupungua mapenzi ya Waingereza kwa mfumo wa kifalme kunashuhudiwa huku familia ya kifalme ya Uingereza ikiwa inakabiliwa na changamoto kubwa kwa miaka kadhaa sasa na kukumbwa na ufisadi mbalimbali wa kimaadili na kifedha. Mbali na hayo, na licha ya madai ya kutoingilia Malkia wa Uingereza na Mrithi wa ufalme katika masuala ya nchi, ukweli unaonyesha kuwa huo ndio uhalisia wa mambo.
Gazeti la Guardian lilitangaza katika ripoti maalumu liliyotoa katikati ya mwaka 2021 kwamba, zaidi ya sheria elfu moja zilipitiwa na Malkia Elizabeth II au mwanawe Mwanamfalme Charles kupitia mchakato wa siri kabla ya kuidhinishwa na Bunge la Uingereza. Sheria hizo zinahusu masuala mbalimbali, kuanzia kujitoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya (Brexit), haki, usalama wa jamii, pensheni, mahusiano ya mbari, sera ya chakula mpaka sheria yenye utata inayohusu ada za maegesho ya magari na ufundi wa ndege…
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *