Wasaudia wengi wapinga kuanzishwa rasmi uhusiano na utawala wa Kizayuni

Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa, asilimia 77 ya wananchi wa Saudi Arabia wanapinga suala la kuanzishwa rasmi uhusiano kati ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Faraan: Gazeti la Arab 21 limeandika kuwa, uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na shirika binafsi la kibiashara la kieneo mwezi Novemba mwaka huu umeweka wazi msimamo wa wananchi wa Saudi Arabia kuhusu baadhi ya masuala ya kimataifa likiwemo suala la kuanzisha uhusiano rasmi kati ya Riyadh na utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo wa maoni, ni asilimia 16 tu ya wananchi wa Saudi Arabia ambao wameitaja suala hilo la kuanzisha uhusiano baina ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni kuwa ni chanya; na mkabala wake, asilimia 77 ya wananchi wa Saudia wanapinga jambo hilo.

Mwezi uliopita tovuti ya Saudi Leaks iliripoti kuwa, tawala za Kizayuni na Saudi Arabia zimefanya mazungumzo kuhusu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya pande hizo mbili licha ya msimamo wa kidhahiri wa Riyadh kuhusu suala la kupatiwa ufumbuzi kadhia ya Palestina.

Safari ya Benny Gantz Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni huko Saudia, safari ya kwanza ya ndege za Riyadh kuelekea Tel Aviv, kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh ndege ya kwanza ya utawala wa Israel, kufikiwa makubaliano kadhaa yenye thamani ya dola milioni mia moja kati ya Tel Aviv na Riyadh na ziara ya ujumbe wa Kizayuni nchini Saudia, ni kati ya hatua zilizochukuliwa katika uwanja wa kuanzisha uhusiano kati ya utawala wa Kizayuni na utawala wa Saudia.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *