Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Mkuu wa shule Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Imetolewa: Msikiti wa Baitul Ateeq
Lahore – Pakistan
2nd Dec. 2022
Hotuba ya 1: Imani iliyofichika husababisha utakasifu, subira na Taqwa (uchamungu)
Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu, na nawasisitizieni kuyasimamisha maisha yenu katika misingi ya Uchaji Mungu.
Tambueni kuwa ucha Mungu ni mjumuiko wa mipango na mikakati kutoka kwa Mwenyezi Mungu yenye kumlinda mwanadamu na pasi na mwanadamu kuwa na Taqwa basi maisha yake yanakua hayana tofauti na yale ya mnyama.
Maisha ya mwanadamu bila ya Taqwa ni sawa na maisha ya wanyama na mfano wake ni maisha ya binadamu katika kizazi cha leo ambapo maadili ya binadamu yamepotea.
Mwenyezi Mungu ameiweka Taqwa katika kila jambo kwa ajili ya usalama wa jambo lile kulingana na sehemu hiyo ya maisha.
Miongoni mwa Sehemu ambayo Taqwa hutumika ni katika uwanja wa vita
Katika Suratul Imran aya ya 123, Allah anasema;
وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّهُ بِبَدْرٍ وَأَنْتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Na Mwenyezi Mungu alikwisha kunusuruni katika Badri nanyi mlikuwa wanyonge. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru.
Mwenyezi Mungu katika aya hii anawaisilisha Taqwa kwa Mtume na maswahaba zake wakati wa vita.
Vita vya Badr ni vita vya kwanza vikubwa ambavyo waisilamu walipambana moja kwa moja na washirikina.
Ingawaje kulikuwa na mapigano madogo kabla ya haya lakini Badr ni vita vya kwanza ambavyo Mtume mwenyewe alikuwepo na akashiriki kwa uwezo wote aliokuwa nao. Vilevile Washirikina walikusanya vikosi vyao vyote na wakaukaribia mji wa Madina kwenye eneo la Badr.
Chanzo cha vita ni pale washirikina walipofanya majaribio yao yote ili kuzuia kuenea kwa Uislamu chini ya uongozi wa Mtume (s.a.w.w) lakini hawakuweza kufikia malengo yao.
Waislamu hawakuwa wanawajibu moja kwa moja kwa kipindi fulani na haya yalikuwa ni mashambulizi ya upande mmoja dhidi ya Waislamu.
Hii ilikuwa ni mbinu ya busara kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na sababu ya msingi ilikuwa kwamba Waislamu kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali hawakuweza kutoa jibu la vita kwa kutumia silaha. Lakini baada ya kufika Madina, walipoungana na Ansari walipata nguvu, walijipanga na kuanza kusimama dhidi ya washirikina.
Kwa kua Washirikina walikua washapora kila kitu kutoka kwa Wahajiri. Msafara ulielekea nchini Syria kwa ajili ya kutafuta bidhaa na washirikina walikua chini ya uongozi wa Abu Sufyan. Mtume (s.a.w.w.) aliamuru kwamba bidhaa hizi zikamatwe.
Washirikina walipopata habari hizo, jeshi jengine lililokua na silaha lilijitokeza kuwakabili Waislamu, Hivyo basi Waislamu walilazimika kukabiliana na vikosi viwili.
Katika hali hii Waislamu walichanganyikiwa na kushindwa kufahamu wa kupigana naye. Quran ilitoa muongozo kwa Mtume (s) ya kua amuache Abu Sufyan na kumtaka apigane na jeshi lile kubwa lililokua na watu 1000 wote wakiwa ni Washirikina.
Hakukuwa na uwiano wa nguvu na Waislamu walikuwa dhaifu ikilinganishwa na kundi la washirikina waliokua na silaha. Waislamu walipoiona nguvu hii walitambua na kuhisi udhaifu wao.
Aya kabla ya hii.
إِذْ هَمَّتْ طَائِفَتَانِ مِنْكُمْ أَنْ تَفْشَلَا وَاللَّهُ وَلِيُّهُمَا ۗ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ
Makundi mawili miongoni mwenu yakaingiwa na woga kuwa watashindwa – na hali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wao; na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.
وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّهُ بِبَدْرٍ وَأَنْتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Na Mwenyezi Mungu alikwisha kunusuruni katika Badri nanyi mlikuwa wanyonge. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru.
Mwenyezi Mungu anasema tulikunusuruni kutokana na hali dhaifu mliyokuanayo katika vita vya Badr.
Kisha baada ya kupewa msaada huu kutoka kwa Mwenyezi Mungu sasa mnapaswa kubwa na Taqwa ili mpate kuwa na shukrani. Hekima iliyomo katika ushindi huu kupatikana ni kuwa na Taqwa mpate kuwa na shukrani.
Shukrani pia kama vile Taqwa ni jambo lenye thamani kwa Waislamu na ubinadamu wote ambao wote wanapaswa kushukuru kwa ajili ya fadhila za Mwenyezi Mungu. Shukr (shukrani) ni kielelezo cha fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Msemo hapa haumaanishi uwasilishaji wa fadhila kwa wengine, bali msemo huu madhumuni yake ni kua fadhila hizo zimetolewa na fidia yake ni shukrani.
Ikiwa Mwenyezi Mungu ametoa mali basi mnapaswa kuitumia mali hiyo kwa lengo ambalo Mwenyezi Mungu ametoa kwa ajili yake na wala msizirundike na kuzificha.
Vile vile neema nyinginezo kama vile afya, umri mdogo na akili ambazo Mwenyezi Mungu ameturuzuku zinapaswa kutumika katika njia iliyo sahihi. Kuwa mwenye shukrani (Shaakir) vilevile inamlazimu mtu kua naTaqwa.
Mtu ambaye si Muttaqee, lakini badala yake akawa ni Fasik, faajir atapoteza fadhila na hawezi kuwa Shaakir. Hatumii fadhila za Mwenyezi Mungu kwa lengo alilolikusudia Mwenyezi Mungu.
Katika umma wetu, Mwenyezi Mungu ametujaalia mali na baadhi ya waumini wanatoa katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa shauku. Wale wanaopata njia hizi, mali zao hawazitumii kwa madhumuni sahihi. Kama ambavyo katika Khums kiasi kikubwa huja kwa wanachuoni na vilevile katika vyuo vya kidini kwa jina la Khums.
Hii ni idadi kubwa na ni sawa na mabilioni ya rupia nchini Pakistani yanayokusanywa kila mwaka japo fedha hizi hazitumiki kwa madhumuni ya Khums.
Waumini wanatoa haki zao na kutoa Khums lakini wanakabiliwa na uzembe huu ambao hawajioni kuwa wanawajibika kuifikisha mahali sahihi inapostahiki kutumika.kwa madhumuni sahihi. Waumini wanadhani kwamba wanapotoa Khums kwenye kituo fulani na chukua risiti basi jukumu lao limekwisha. Kisheria sio hivyo, anapokupa kodi au Khums na akachukua risiti basi jukumu lake limekwisha.
Lazima utoe majukumu yako ya kibiashara na unapaswa kuyafanya yafikie mahali ambapo una uhakika kwamba utajiri huu utatumika katika njia iliyosahihi. Ikiwa huna ushahidi wowote kwamba hii inatumiwa kwa madhumuni sahihi basi wajibu huu haujafikishwa.
Kushukuru kwa fadhila ni kuzitumia kwa madhumuni yake sahihi. Nchini Pakistani watu wanatoa Khums tangu muda mrefu na ninaweza kutoa mfano katika hili; Allama Mufti Jafar aliasisi madrassa yake kabla ya miaka ya 80.
Waumini walikuwa wakiiunga mkono madrasa hiyo tangu wakati huo. Walikuwa wakitekeleza wajibu wao ingawa wengine waliporakutoka kwenye hazina ya umma.
Ukihesabu ni kiasi gani cha mali kilichoporwa na Banu Umayyah na Banu Abbas ukilinganisha na mali iliyoporwa na wafuasi wa Ahlulbayt (a), utaona kwamba watu wa zama hizi wamefanya uporaji wa mali kiasi kikubwa zaidi ikilinganishwa na zama zile.
Hatuwezi kuwalaani watu hao kwakua tunayoyafanya hayana tofauti na waliyoyatekeleza. Wale wanaotoa hawajifikirii kuwa ni wajibu kwao kuhakikisha inatumika wapi.
Wale waliokuwa wakimpa Allama Mufti Jafar wakati huo waliendelea kutoa na baada ya Madrassah kuwa katika hali mbaya na kuharibika na kusimamishwa vievile bado waliendelea kutoa.
Kisha baada ya hapo tukaanzisha tena Madrassa na vilevile bado pesa ilikuwa inatumwa kwenye akaunti ya zamani na wahudumu wapya hawakuwa na uwezo wa kuingia kwenye akaunti hiyo.
Akaunti hiyo ilipozuiwa kutokana na ukaguzi wa serikali, kiasi cha pesa kilichokuwemo pia kilizuiwa. Huu ni mmoja kati ya mifano ya kiutendakazi nilioutoa hapo mwanzo ambapo watu wanaendelea kutoa mali zao pasi na kutathmini matumizi yake.
Madrassa ilisimama lakini msaada huu uliendelea na hakuna yeyote aliyechukua kiasi hicho na vipi kilitumika kwa sababu matumizi ya Madrassa hiyo hayakuonekana.
Nimesema hivi kwa sababu wanaotoa hawatambui wala kutathmini ni wapi mali hiyo inatumika. Shukr maana yake ni kutumia fadhila katika mwelekeo ambao Mwenyezi Mungu ameutoa.
Shukrani hii inafanywa na nani? Yule ambaye ni Muttaaqqee anatumia fadhila katika mwelekeo sahihi. Muttaqqee ndiye ambaye ameyalinda maisha yake kutokana na hatari zote. Mtu ambaye ni mfisadi na mpotovu hana shukrani.
Katika Aya hii Mtume anaambiwa kwamba sisi tumekunusuruni katika Badr mlipokuwa dhaifu sana. Kuna amri kwamba baada ya kufaulu kwa Badr inabidi upate Taqwa ili uwe mwenye kushukuru.
Katika vita vya Badr hali ya Waislamu ilikuwa na hofu. Kikosi hiki cha watu 300 walipoona vikosi hivyo walishtuka kwani hawakuenda vitani, walikuwa wametoka kuchukua ngawira.
Badala ya msafara wa wafanyabiashara wanaposema kikosi cha silaha walikuja chini ya shinikizo. Mtume (s) alikuwa akishutumiwa kwamba hukutuambia jambo sahihi; ya kwamba aliwatoa kwa ajili ya kitu kingine na kutuingiza kwenye shida hii.
Mtume (s.a.w.w.) akawaambia haitoshi kwamba Mwenyezi Mungu atakunusuruni kupitia Malaika wake. Alisema malaika 3000 watashuka kwa ajili ya msaada wenu.
إِذْ تَقُولُ لِلْمُؤْمِنِينَ أَلَنْ يَكْفِيَكُمْ أَنْ يُمِدَّكُمْ رَبُّكُمْ بِثَلَاثَةِ آلَافَةِ آلَاثَةِ آلَاثَةِ آلَاثَةِ آلَفَكُمْ رَبُّكُمْ بِثَلَاثَةِ آلَاثَةِ آلَاثَةِ آلَاثَةِ آلَفَكُمْ يُمِدَّكُمْ
Ulipo waambia Waumini; Je, haitkutosheni ikiwa Mola wenu atakusaidieni kwa Malaika elfu tatu walio teremshwa?
بَلَىٰ ۚ إِنْ تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا وَيَأْتُوكُمْ مِنْ فَوْرِهِمْ هَٰذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّفَةِكُمْ رَبُّفَلَكُمْ رَبُّفَةِكُمْ رَبُّفَةِكُمْ رَبُّمُمْ رَبُّمْكُمْ فَوْرِهِمْ فَوْرِهِمْ هََٰا يُمْدِدْكُمْ رَبُّفَةِكُمْ رَبُّفَلَكُمْ رَبُّفَةِكُمْ رَبُّفَةِكُمْ رَبُّكُمْ رَبُّكُمْ فَعَلَى
Kwani! Ikiwa mtavumilia na mkamchamngu na hata maadui wakikutokeeni kwa ghafla, basi hapo Mola wenu Mlezi atakusaidieni kwa Malaika elfu tano wanao shambulia kwa nguvu.
Hali hii haikua katika uwanja Badr pekee bali inatumika katika makabiliano yoyote katika kila zama. Umma wowote utakaosimama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa subira na Taqwa, basi Mwenyezi Mungu atawaunga mkono kwa njia ya ghaibu ambayo inaweza kuwa kwa njia za kimwili na zisizo za kimwili.
Hii ni sheria ya kawaida ya Mwenyezi Mungu ambayo inapaswa kujaribiwa. Waumini wanapaswa kupata Taqwa na subira kisha wasimame dhidi ya nguvu yoyote ile kubwa itakayokua dhidi yao, basi hakika Mwenyezi Mungu atawanusuru waumini hawa kama alivyowasaidia katika Badr.
Kwa kuwa tumefundishwa Quran kwa namna tofauti. Leo pia Badr yupo ambapo wachache wa waumini wanasimama dhidi ya jeshi kubwa. Wakati makabiliano kama haya yanapotokea, wanaunga mkono Taghoots.
Nchini Pakistan Mashia ni wachache. Wachache hawa kwa ajili ya uhuru wa imani yao wanakabiliwa na magumu kutoka kwenye nguvu za ubaguzi, za kitakfiri.
Ili kukabiliana na vikosi hivi, uongozi uliopo ndani yetu umeonyesha fomula ya kupata kimbilio kutoka kwa baadhi ya Taghoot zenye nguvu, jiunge nao na kwamba Taghot itakulinda dhidi ya takfiri na magaidi.
Umekuwa na Taghoot na kuona kuwa wao wenyewe sio salama kwa hivyo itakuwaje wawe walinzi wako. Unaungana nao kwa ajili ya usalama na hata hawahudhurii mazishi ya mashahidi.
Mnakaa mtaani siku nyingi miili na familia zao zikitetemeka lakini akina Taghoot wanawatukana kwa kusema kuwa wewe ni mweusi unatutumia barua za mashahidi. Huu ndio mtindo ambao tumeubadilisha kwa kuwa sisi ni wachache tunapaswa kutafuta ulinzi kupitia Taghot.
Mwenyezi Mungu anasema katika Badr mlikuwa wachache bila silaha yoyote. Mambo mawili yalikuwepo kwa baadhi na hasa kwa kiongozi wao na masahaba wachache waliochaguliwa.
Kama katika Ohud ilionekana ni wangapi walionyesha uvumilivu. Quran imewasilisha desturi hii kwamba ikiwa watu wachache wana subira na Taqwa basi nusura ya Mwenyezi Mungu inakuja.
Mwenyezi Mungu aliwanusuru katika Badr katika hali dhaifu. Mwenyezi Mungu alikunusuruni kwa sababu kiongozi wenu alikuwa na imani kwanza juu ya msaada huu wa Mwenyezi Mungu na pili zile kanuni mbili za subira na Taqwa ikachukuliwa naye hivyo Mwenyezi Mungu akamjaalia mafanikio.
Unaweza kuona kwamba Mashia wa Lebanon ni dhaifu kuliko Mashia wa Pakistani. Nchini Lebanon hata miongoni mwa Mashia sio wote wanaounga mkono harakati ya Hizbollah, wengine wanapinga harakati hiyo na kushikamana na vyama vingine.
Harakati ndogo kama hii ilipewa heshima na Mwenyezi Mungu dhidi ya Waarabu, ISIS na Amerika. Kama ilivyokuwa katika vita vya Badr, wakizingatia nukta hii ya Taqwa, subira na imani kuhusu msaada wa Mwenyezi Mungu.
Hivyo basi jumuiya nyingine nazo zinapaswa kuwa na imani juu ya hili, na kuelewa siri hii kwamba tutegemee msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Yeye hawaungi mkono MaTaghot bali kupitia jeshi lake mwenyewe la Malaika.
Hotuba ya 2: Wasomi wanaoamiliana na Taaghut hawawezi kamwe kusimamisha utawala wa Kimungu
Imepokelewa kutoka kwa Amirul muminin katika hekima nambari 110 :
وَ قَالَ (علیه السلام): لَا يُقِيمُ أَمْرَ اللَّهِ سُبْحَانَهُ إِلَّا مَنْ لَا يُصَانِعُ وَ لَا يُضَارِعُ وَ لَا يَتَّبِعُ الْمَطَامِعَ.
“Utawala wa Mwenyezi Mungu aliyetakasika kamwe hauwezi kusimamishwa isipokuwa na yule ambaye hakengeuki katika jambo la haki, ambaye hafanyi kama wafanyavyo madhalimu, na wala hafuati matamanio yake.”
Mtu asiyekengeuka katika jambo la haki, asiyefanya kama wafanyavyo madhalimu, na wala hafuati matamanio yake. Hawezi kabisa kuwa sawa na yule ambaye ana mapungufu haya matatu.
Kwani huyu wa pili kamwe hawezi kuanzisha utawala wa kiungu.Sifa ya kwanza ni Musanah, Mudahna maana yake ni kuafikiana. Hakubaliani na ukweli na maadili.
Haya ndiyo maadili ambayo yaliwaweka watu mbali na Amirul Momineen (a) hasa katika zama zake. Kama makundi yaliokuwa dhidi ya Amirul Momineen (a), yalikuwa na sifa moja iliyoiwapambanua na wahusika wengine nayo ni kwamba waliweza kufanya kila lililokuwa katika uwezo wao almuradi tu wafikie uongozi.
Walifungua milango yoyote ile na kuwezesha njia zozote zile zilizoweza kutumika zitumike sawa sawa ziwe ni za haramu, uongo, unyang’anyi, n.k.
Watu hawa walijiliwaza kwa kujiambia kuwa, baada ya kuingia madarakani tunachokitaka sisi ni hatimaye tuweze kupata fursa ya kuitumikia jamii, jambo ambalo ni jema na linalohalalisha njia zisizo halali zilizotumika kufikia madaraka.
Kwa hivyo wakawa wanafundisha kwamba unapaswa kuondoa vizuizi vyote vile vyenye kumzui mtu kuingia madarakani. Huu ndio mfumo na njia isiyokuwa sawa iliyotumika na ambayo kwayo mamlaka yalinyakuliwa kutoka kwa Amirul Momineen (a).
Leo hii ni dhahiri shahiri kuwa siasa zilizopo kote ulimwenguni zinaonekana kumruhusu mtu kufanya jambo lolote lile liwe la halali na lisilo kuwa la halali almuradi tu kuingia madarakani.
Hata ikibidi kuafikiana na madhalimu, kusema uwongo, kuunga mkono Taghut, au muungano na mtu basi hakikisha unafanya haya yote, kwani lengo loa msingi na inayokubidi kuangalia ni njia ngapi zipo za kuingia madarakani na wala usizingatie kabisa kama zenyewe ni nzuri au mbaya. Wakati fulani watu kama hao huingia madarakani pia ambao hutumia kila linalowezekana kama njia.
Mfano wa wazi wa hili nchini Pakistan ni serikali iliyopita ambayo ilitumia kila mbinu kuingia madarakani. Waliingia madarakani wakiwa na kauli mbiu zote kubwa za kukomesha ukosefu wa haki, umaskini, ajira, na ukosefu wa makazi hivi kwamba waliahidi hata watu wengine wasiokuwa wapakistani watakuja Pakistan kutafuta ajira.
Hizi zote zilikuwa kauli mbiu zilizotolewa almuradi tu wapate kuingia madarakani. Na kwa kweli Waliingia madarakani kwa kauli mbiu, lakini kilichofuatia, na uchafu uliokuwepo leo hii umefichuliwa.
Watu hawa walijizatiti kwa njia yoyote ile iliyowezekana kuingia madarakani, basi tazama katika kila nyanja, je kunacho walichokifanya? Hata waulizapwo wenyewe hawana jibu, majibu waliobakisha ni kusema kwamba wengine pia ni mafisadi, na majambazi.
Na utakuta wanaosikiliza wanaridhika kwamba kwa vile wengine ni wachafu vivyo hivyo na sisi pia tusiwalaumu. Je, ni mwelekeo gani huu tuliouchukua ambao ili mtu kufikia madarakani huruhusiwa hutumia kila mbinu ziwe nzuri, au mbaya?
Amirul Momineen (a) anaeleza siri kubwa na ukweli; anatufundisha siasa. Hii ni siasa ya Ali (a). Tukitazama kwa makini makundi yote ya kidini katika nchi yetu yawe ya Kishia au Kisunni katika siasa, utakuta wote wanatumia dini kwa njia zisizo kuwa za kidini.
Unapotumia dini, basi sharia, mfumo wa Mtume, Quran, na Uislamu zitakuwa kauli mbiu. Wanapeperusha kauli mbiu za namna hii ili waingie madarakani kisha baadaye wafanye chochote wanachotaka kukifanya.
Wale waliowaamsha wananchi hata hawakumbuki ni uongo gani aliousema kabla ya uchaguzi na anafanya nini sasa.
Wanasiasa wanaichukulia Pakistan kama mbingu na iishio watu wasio kuwa na akili. Ni pepo kwa kila mfuasi, mwongo, na mwenye nia mbaya. Watu wa aina hii ndio watakaingia madarakani, na utawakuta juu ya mimbari, na katika nguzo muhimu za kukamata na taifa.
Haya yote yatatokea katika paradiso hii ya watu wasio na akili.
Katika bayana ya Ali (a) anasema kwamba ikiwa unachukulia utawala wa Allah kuwa ni jambo lenye umuhimu basi tazama kwa makini ni nani anayeweza kuchukua na kutekeleza kwa uzuri jukumu hili.
Ndiposa akazitaja sifa hizi kuwa kwanza anapaswa kuwa mtu asiyekubali kubadili ukweli kwa kitu chochote kile. Kuridhiana maana yake ni kutoa na kukubali kubadilika badilika kwa ukweli, na kukubali uwongo fulani ili kufikia lengo.
Kitendo hiki hakipendi Amirul Muminin (a) kitendo ambacho kinahesabika kuwa ni hadaa na watu kama hao hawawezi kamwe kusimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu.
Msemo huu unatufanya kuelewa historia nzima hapa. Na sababu kuu iliyopelekea Mfumo wa Uimamu kutoimarika katika historia nzima kwa kuwa wale wote waliokuwa wakishikilia vyeo vya uongozi walikuwa ni wenye kufanya maridhiano na kukubali kubadili baadhi ya kweli na leo pia viongozi wenye fikra hii wapo.
Sifa ya pili ya mtu anayeweza kusimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu ni wale ambao ni Ahle Muzareya. Maana ya neno hili ni wale wanaokubali fedheha na unyonge.
Watu wenye sifa hii katu hawawezi kusimamisha amri ya Mwenyezi Mungu. Maana ya pili ambayo ndio kauli ya wengi wa wanachuoni ni Mushabehat (kuiga) ambayo ina maana ya watu ambao wanapoingia katika mazingira fulani, wanakuwa kama angahewa.
Badala ya kubadilisha jamii, wanabadilika wao na kujipamba na sifa za kwao. Wanapokaa na waovu wanakuwa kama wao, na wakiwa na watu wema wanakuwa wema. Ni kama Kinyonga wanaobadilika rangi kulingana na mazingira.
Watu hawa wanaogeuka geuka hawawezi kumsimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu. Walengwa wakubwa wa Amirul-Muminin (a) katika msemo huu ni wanachuoni kama vile utawala wa Mwenyezi Mungu inavyothibitishwa kupitia wanachuoni.
Wakati wasomi ni waathirika wa magonjwa haya. Unapoingia kwenye anga chafu basi kuna fedheha katika anga hilo.
Mfano mmoja ni katika Fiqh kwa kila mtu makhsusi kwa wanachuoni. Mfano kwamba mnyama fulani au binadamu akianguka kwenye mgodi wa chumvi na kufia humo. Ulipata habari kwamba hii ilitokea na mtu na sasa unaenda huko kumtafuta.
Utastaajabu kwa kukuta hakuna kidokezo cha mwili hapo, na chumvi pekee ndiyo itaonekana hapo. Huu ndio ubora wa chumvi ambayo kitu chochote kikianguka kwenye chumvi huwa chumvi.
Wanachuoni wanatoa mfano huu katika sura ya utakaso na katika istilahi, inajulikana kwa jina la Istehala. Hii ina maana ya mabadiliko ya hali moja hadi nyingine kabisa kwa kupata umbo, na sura ya kitu kingine.
Wanazuoni hupitia Istehala wanapoingia katika mazingira tofauti. Wanakuwa Malang, Chaudhary, Gaali, na Nasibi walipoingia kwenye angahewa kama hizo. Tashabuh ni jina la Istehala hii.
Yule ambaye ameandikiwa kusimamisha amri ya Mwenyezi Mungu lakini amerekebisha na akabadilika kwa hali. Wengine wamuongoze pia aende kulingana na hali.
Hakuna anayesema endelea kuwa na msimamo na usiwe na shinikizo, usiwe kama wao badala yake wabadilishe. Walimuonea huruma Imamu Husein (a) na wakamuomba ingawa asiwe kama Yazid bali awe kama hawa Haji hawa kimya, watu wa Madina na Kufa.
Kwa nini usichukue rangi ya mtu mwingine? Imam hakufanya Istehala mwenyewe.
Wengine walikuwa watu wazuri lakini walipitia istehala. Wanabadilika na kuwa kama wengine. Wanachukulia marekebisho haya kama sifa nzuri. Makubaliano haya mawili na marekebisho ni laana za Ali. Ikiwa kiongozi anaweza kuafikiana, na kurekebisha basi mtu huyu hawezi kuanzisha Amr e Ilahi.
Sifa ya tatu ni mtu mwenye maslahi binafsi, hawezi kuanzisha Amr e Ilahi. Yule ambaye hana masilahi mengine ya kibinafsi isipokuwa Amr e Ilahi anaweza tu kufanya hivi.
Tatizo kubwa la Maimamu lilikuwa ni kwamba hawakuzoeana na wengine. Lakini wale waliojirekebisha au kuridhiana waliuona ulimwengu kwa siku chache lakini wakabaki wahalifu mbele ya Mwenyezi Mungu.
Wanachuoni walichukua tawala mikononi mwao ili kuanzisha Amr e Ilahi. Ikiwa mtu ni Marjae Taqlid na anafanya maelewano basi vipi anaweza kuliongoza taifa? Ikiwa anaogopa Azadar, Malang na maelewano na kila mtu basi anawezaje kuwafundisha wengine dini? Ataharibu dini. Na pili, ikiwa atabadilika na kuwa kama wengine. Anapowaona watu wa magharibi anakuwa kama wao.
Kwa ajili ya kuufurahisha utamaduni wa kimagharibi, Marekani, wabadili mtazamo wao na pia wa dini.
Amirul Muminin (a), na Imamu Husein (a) hawakuwa na chochote cha kuridhiana. Tunaposema kwamba Imamu Hassan (a) alifanya suluhu, basi mimi nimeeleza haya, ambayo unaweza kusoma katika tabrisi ambaye alifanya suluhu hii. Imam Hassan (a) alipoona ramani ya wale walioafikiana na maadui alibuni mbinu hii.
Makufi, kamanda mkuu wa jeshi lake, Mashia. Walifanya suluhu kwamba tutamkabidhi imam Hassan kwa Muawiya. Imam aliwalinda Mashia, dini, na Ahlulbayt (a) kutokana na mapatano haya. Hawakuruhusu Amr e Ilahi kuanzishwa.
Wakati wowote Ali alipojaribu kusimamisha Amr e Ilahi, watu walioachana walijitokeza kumzuia. Kwa kuwa ni takatifu, hazihesabiwi. Wanafikiri kwamba hakuna mtu anayeweza kusimama mbele ya utakatifu wetu.
Amirul Momineen (a) alisema kwamba hakuna mtu mwingine zaidi yangu anayeweza kupigana na Khawarij. Hii ndiyo Taqwa ya kivitendo iliyoelezwa na Amirul Momineen (a).