Ukoloni wa Uingereza ulikuwa sababu ya vifo vya zaidi ya watu milioni mia moja nchini India.
Kapil Kumar, mtaalamu wa masuala ya kihistoria wa India, amesema kwenye televisheni ya Russia Today kwamba: “Kulingana na utafiti uliofanywa katika karne za 19 na 20, vitendo vya kikoloni vya Uingereza nchini India vilisababisha vifo vya watu milioni 165 katika nchi hiyo, idadi ambayo ni kubwa zaidi ya jumla ya wahanga wa vita viwili vikuu vya dunia.”
Mtaalamu huyo wa historia ya India amesema: Haya ndiyo mauaji makubwa zaidi katika historia ya mwanadamu, na Uingereza imekuwa na nafasi kubwa katika mauaji ya halaiki nchini India.
Utafiti huo unaonyesha kuwa, katika miaka ya ukoloni wa Waingereza nchini India, dola trilioni 45 mali ya nchi hiyo ziliibwa na kuporwa na Waingereza.
Kapil Kumar ameongeza kuwa, ukoloni wa Uingereza ulikuwa na athari mbaya kwa India, ambazo zilisababisha umaskini uliokithiri na kuongezeka kwa vifo.
India ilipata uhuru na kujitawala kutoka kwenye makucha ya mkoloni Mwingireza tarehe 15 Agosti 1947.