Watu 137 wauawa katika siku ya kwanza ya vita vya Ukraine

Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amesema kuwa, watu 137 wameuawa katika siku ya kwanza tu ya vita vya Russia nchini mwake.

limemnukuu Zelenskyy akisema hayo mapema leo Ijumaa na kuongeza kuwa, tangu vilipoanza vita vya pande zote za Russia dhidi ya nchi yake, watu 137 wameshauawa na 306 wamejeruhiwa katika kipindi cha chini ya masaa 24 yaliyopita.

Vile vile amelalamika kuwa nchi za Magharibi za Ulaya na Marekani zimeiacha mkono nchi yake na hivi sasa Ukraine iko peke yake katika kukabiliana na Russia.

Rais huyo wa Ukraine ametoa mwito kwa wananchi wa nchi hiyo wajilinde wenyewe na wasitarajie msaada wa kijeshi kutoka nchi za Magharibi.

Jumatatu ya tarehe 21 Februari, Russia ilitangaza kutambua uhuru wa majimbo mawili ya Donetsk na Luhansk katika eneo la Donbas, mashariki mwa Ukraine baada ya nchi za Magharibi kutojali usalama wa kitaifa wa Russia.

Jana Alkhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilisema kuwa, imeamua kuanzisha operesheni maalumu ya kijeshi nchini Ukraine ili kuzuia kutokea vita vikubwa vya dunia.

Aidha akizungumza na televisheni ya “Rusia 24,” Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, lengo la nchi yake si kuliangamiza jeshi la Ukraine bali ni kudhooofisha uwezo wa kijeshi wa nchi hiyo na kuhakikisha kuwa usalama wa Russia unalindwa kwa kuyazuia madola ya Magharibi na NATO kukusanya majeshi yao katika mipaka ya Russia.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *