Watu 28 wauawa katika mashambulizi ya jeshi la Ethiopia

Vyombo vya habari vimewanukuu wanamgambo wa kundi la Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray wakisema kuwa mashambulizi ya anga ya ndege za jeshi la Ethiopia yameua watu 28 na kujeruhi wengine 76 katika mji mmoja wa kaskazini mwa nchi hiyo.

Faraan: Msemaji wa Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) amesema kuwa, watu 28 wameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na jeshi la Ethiopia katika soko moja kwenye mji wa Alamata.

Hadi sasa hakujatolewa taarifa zaidi kuhusiana na madai hayo.

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilitatarajiwa kukutana mjini Geneva leo Ijumaa kwa kikao cha dharura kinachojadili uhalifu wa kivita unaofanywa na pande zinazopigana nchini Ethiopia.

Mapigano katika jimbo la Tigray yanashadidi katika hali ambayo, indhari mbalimbali zimeendelea kutolewa kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu katika jimbo hilo.

Vita hivyo vya kaskazini mwa Ethiopia vimepelekea maelfu ya watu kuuawa, zaidi ya milioni mbili kuwa wakimbizi na kuwafanya mamilioni ya wengine kukabiliwa na baa la njaa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *