Waziri Mkuu wa Lebanon: Hizbullah ina haki ya kufanya shughuli zake sawa kabisa na vyama vingine vya siasa

Waziri Mkuu wa Lebanon amesema kuwa harakati ya Hizbullah iko sawa kabisa na vyama vingine vya siasa vya nchini humo kwa kuwa ni chama cha siasa.
Akizungumza leo katika mkutano uliofanyika ikulu ya Waziri Mkuu, Najib Miqati Waziri Mkuu wa Lebanon amebainisha kuwa Lebanon inakabiliwa na matatizo na vitisho vingi na vikubwa; na hakuna njia nyingine ya kuondokana na matatizo hayo ghairi ya kusimama imara na kusaidiana kwa pamoja. Miqati amesisitiza kuwa, kama kujiuzulu kwake kungekuwa kwa maslahi ya Lebanon basi bila shaka angefanya hivyo lakini katika mazingira ya sasa hatua hiyo itaifanya hali ya mambo nchini humo izidi tu kuwa tata.

Waziri Mkuu wa Lebanon ameongeza kuwa, serikali ya nchi hiyo haijafanya mkutano wowote katika ngazi ya mawaziri tangu tarehe 12 Oktoba hadi sasa; na jambo hilo kimsingi limeathiri utendaji wa serikali, na katika upande mwingine hawezi kumhusisha yoyote na suala hilo. Amesema Harakati ya Hizbullah kama vilivyo vyama vingine vya siasa huko Lebanon inaweza kuendesha ghughuli zake; na kwamba hakubaliana na wazo kwamba Lebanon inadhibitiwa na kuhodhiwa na nyingine zingine.

Waziri Mkuu wa Lebanon ametangaza kuwa, amesaini mpango wa kuitisha uchaguzi wa bunge mwezi Mei mwakani. Amesema tayari mpango huo umeshakabidhiwa kwa Rais ili kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kama ilivyopangwa.

Wabunge wa Lebanon wametangaza kuwa uchaguzi wa bunge nchini humo utafanyika Machi 27 mwaka ujao wa 2022.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *