Waziri Mkuu wa Niger alisema kuwa Marekani inahusika na kusambaratika kwa uhusiano kati ya Washington na Niamey, na akasema: “Washington haina haki ya kututaka kukata uhusiano na Iran na Russia.”
Kwa mujibu wa ripoti hii, Ali Mohman Lamin Zain aliishutumu Marekani kwa kuruhusu magaidi kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Niger, na Washington haikuilinda nchi yake dhidi ya ugaidi.
Waziri Mkuu wa Niger amesisitiza kuwa, serikali ya Marekani haina haki ya kuitaka nchi hii kukata uhusiano wake na Iran na Russia.
Baraza la kijeshi la Niger mwezi Machi mwaka jana lilifuta makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani ambapo wanajeshi wa Marekani walikuwepo Niamey.
Kufuatia hatua hii, Marekani ilikubali kuondoa takriban wanajeshi 1,000 kutoka Niger mwezi Aprili.