Waziri wa mafuta wa Yemen aonya makampuni ya kigeni dhidi ya uporaji mafuta, gesi

Waziri wa mafuta na madini katika Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen amezionya kampuni za kigeni dhidi ya kupora utajiri wa mafuta na gesi ya nchi hiyo ya Kiarabu inayokumbwa na vita, na kusisitiza kwamba Sana’a haitaacha juhudi zozote za kutetea mamlaka ya kitaifa na kulinda maslahi na utajiri wa umma.

Ahmed Dares ameyataka makampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi kuingia katika mazungumzo na serikali ya Sana’a kabla ya kuchukua hatua zozote za kuchunguza na kuchimba mafuta ghafi na gesi asilia nchini Yemen, na kuonya madhara mabaya endapo onyo hilo halitazingatiwa kwa uzito.

Waziri wa Mafuta wa Yemen amesema nchi yake haitakaa na kuwa mtazamaji wakati  muungano vamizi  unaoongozwa na Saudi Arabia unaendelea kuhujumu uchumi wa nchi.

Mwishoni mwa Oktoba, Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen ilitoa onyo baada ya kulenga meli ya mizigo kutoka kwenye kituo cha mafuta kusini mwa nchi hiyo ili kuzuia vikosi vinavyoungwa mkono na Saudia kuitumia kwa mauzo ya mafuta yaliyoporwa.

Wizara hiyo ilisisitiza kuwa Yemen haitasita kutetea mamlaka ya kitaifa, na kulinda maslahi ya umma na utajiri dhidi ya kitendo chochote cha uporaji.

Mwezi Novemba pia, wanajeshi wa Yemen na wapiganaji waitifaki walifanikiwa kusimamisha meli ya kigeni ya mafuta kwenye maji karibu na Mkoa wa kusini mwa Shabwah wenye utajiri wa nishati ilipokuwa ikijaribu kusafirisha mamia ya maelfu ya mapipa ya mafuta yaliyokuwa yanaparowa kutoka kwa taifa hilo masikini la Kiarabu.

Saudi Arabia ilianzisha vita vikali dhidi ya Yemen mwezi Machi 2015 kwa ushirikiano na washirika wake wa Kiarabu na kwa msaada wa silaha na vifaa kutoka Marekani na mataifa mengine ya Magharibi.

Lengo lilikuwa kuuweka tena utawala kibaraka wa Riyadh wa Abd Rabbuh Mansour Hadi na kkuondoa madarakani vuguvugu la Ansarullah linalopata uungaji mkono wa wananchi.

Wakati muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umeshindwa kufikia malengo yake yoyote, vita hivyo vimeua mamia ya maelfu ya Wayemeni na kusababisha mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *