Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa Iran imeacha wazi dirisha ili kufikia mapatano lakini dirisha hilo halitasalia wazi siku zote. Amesema Iran inakaribisha na kuunga mkono ubinifu wa Mfalme wa Oman ili kufanyika ufatiliaji kwa lengo la kufikia mapatano mazuri, imara na endelevu.
Hossein Amir- Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Oman amesema kuhusu natija ya ziara yake katika nchi ya Kiarabu ya Oman baada ya baada ya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa serikali ya nchi hiyo kwamba: katika ziara yake hiyo wamejadili na kubadilishanamawazo kuhusu baadhi ya masuala ya kieneo na kusisitiza kuhusu umuhimu wa amani, uthabiti na ustawi katika eneo kupitia kushirikiana nchi za eneo.
Wakati huo huo,kuhusu mazungumzo ya kuondoa vikwazo na uhusiano wa ziara yake hiyo na mazungumzo na nyuklia ya Iran na nafasi ya Oman katika uwanja huo, Amir-Abdollahian amesema: Umoja wa Ulaya unaendeleza jitihada zake kama Mratibu wa kufanikisha mazungumzo ya nyuklia hasa ikizingatiwa kuwa Oman tangu awali ilikuwa mpatanishi mkuu ili kufikiwa mapatano mwaka 2015; na katika miezi kadhaa iliyopita pia imeendeleza jitihada zake kubwa katika uwanja huo na jitihada hizo zinaendelea hadi sasa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa: katika mazungumzo na viongozi wa Oman wamesisitiza kuwa, iwapo pande nyingine katika mazungumzo hayo hazitaacha unafiki na Wamagharibi kutozingatia uhalisia wa mambo hakuna uhakika kwamba dirisha lililoachwa wazi hii leo ili kuendeleza mazungumzo litasalia wazi pia hapo kesho.