Waziri wa ulinzi wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemeni alisema kuwa “Hifadhi ya nchi ya silaha za balistiki na za kimkakati zinatosha kwa vita vya miongo mingi,”
Kwa mujibu wa kituo cha Televisheni ya Al-Masira ya Yemen, Jenerali Mohammad Nasser Al-Atefi aliongeza siku ya Jumamosi: “Tunakubaliana na amani ambayo itahakikisha maslahi ya juu ya watu wa Yemen na heshima na uhuru wa nchi.”
Alibainisha kwamba: “Tunawatangazia na kuwaonya wavamizi wanaoongozwa na tawala za Saudia na Imarati, kuondoka na kuachana na Yemen na kutowachokoza wanajeshi wa Yemen, kwa sababu wanajeshi wetu wanajua jinsi ya kuwaadhibu na kuwatia adabu wale ambao bado mpaka sasa hawajajifunza.”
Al-Atefi amesema: “Iwapo adui hatasikiza nasaha nzito na za kweli za Wayemen, wanapaswa kujilaumu wenyewe, kwa sababu sisi hatuwajibiki kwa uziwi wao na kujisalimisha kwao kwa miji mikuu ya Magharibi na Mazayuni.”
Amewataka wavamizi kusikiliza nasaha za mara kwa mara za kiongozi wa Ansarullah na kuelewa maana yake, na kuachana na watu wa Yemen, vinginevyo watajuta.
Waziri wa Ulinzi wa Yemen amesema: “Iwapo hawatasikiliza ushauri wa uaminifu, tutafanya jambo ambalo litawaliza na maombolezo yao yajae duniani, na kisha majuto yao yatakuwa ya bure na hakuna mtu wa kuwaokoa na kuwalinda na mapigo yetu.”
Aliongeza kuwa: “Tumeongeza sehemu muhimu za ndni na muhimu katika nchi zilizovamia Yemen, na tutawashangaza kwa mapigo ya aina yake ikiwa hawataacha uchokozi na mzingiro ya nchi ya Yemen.”
Al-Atefi aliongeza: “Sekta ya kijeshi na wahandisi wa kijeshi wanafanya kazi usiku kucha ili kuimarisha na kupanua hifadhi ya makombora ya kimkakati ya balestiki na ndege zisizo na rubani zenye ufanisi katika vita vya muda mrefu.”
Amesema: “Tunawausia madui na wafuasi wao wasiepima subira yetu kwa sababu tunaweza kuwapiga mapigo yenye uchungu.