Waziri wa Ulinzi Yemen: Uporaji wa mali ya Yemen hautapita bila jibu

Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen ameashiria njama za muungano wa vita wa Saudi Arabia za kupora utajiri wa Yemen na kusisitiza kuwa operesheni ya uporaji wa mali ya Yemen haitapita bila jibu.

Yemen ni moja ya nchi ambazo zina mapato ya nishati, ingawa ni ndogo na vyanzo vya nishati vya Yemen viko katika majimbo ya kusini kama vile Shabwah na Hadhramaut, majimbo ya kaskazini kama vile Marib na Al-Jawf, na baadhi ya majimbo ya mashariki.

Hivi karibuni, mafuta na gesi ya mkoa wa Shabwah wa Yemen yamekuwa yakiporwa na nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Ufaransa. Mnamo Julai mwaka huu, meli ya mafuta ya Imarati ilipakua mapipa 400,000 ya mafuta yasiyosafishwa yenye thamani ya zaidi ya dola 43,640,000 kutoka bandari ya Razum katika jimbo la Shabwah.

Kabla ya hapo, zaidi ya mapipa milioni mbili ya mafuta ghafi yenye thamani ya takriban zaidi ya dola milioni 270 yaliporwa kutoka bandari ya Al-Shahr katika mkoa wa Hadramaut nchini Yemen.

Mohammed Nasser al-Atafi, Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen, amesema kuwa hatua ya muungano wa vita wa Saudia ya kutoheshimu usitishaji vita ni kielelezo cha azma ya ukoloni wa nchi za Magharibi ya kupora mali ya Yemen, na kufafanua kuwa, Sana’a inaelewa vyema mipango na njama za wavamizi za kupora rasilimali ya mafuta na gesi ya Yemen.

Al-Atafi ameongeza kuwa, uporaji wa mali ya Yemen hautapita bila jibu na vita vya ukombozi na uhuru vinaendelea hadi wavamizi hao watakapotimuliwa kikamilifu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *