Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni atishia kujiuzulu

Waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni alitoa onyo kwa baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni ya kwamba atajiuzulu iwapo mageuzi ya mahakama yatafanyika.

Yoaf Gallant, Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni alitishia kujiuzulu kwa baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu siku ya Jumatatu.

Kanali ya 13 ya utawala wa Kizayuni imeripoti kuwa Waziri wa Vita wa Kizayuni ametishia kujiuzulu iwapo baraza la mawaziri litatekeleza kwa upande mmoja mabadiliko yanayohusiana na mfumo wa mahakama katika utawala huo.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwaambia mawaziri wake mapema kwamba ikiwa hawatafikia makubaliano na “upinzani” kuhusu mabadiliko ya mahakama, uwezekano wa Gallant kujiuzulu ni mkubwa sana.

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti leo kwamba kwa muda wa wiki mbili zilizopita, “mazungumzo magumu” yamekuwa yakiendelea nyuma ya pazia kati ya Netanyahu na Gallant. Katika mazungumzo hayo, Gallant alielezea hali halisi ya jeshi la Kizayuni na taasisi zake za usalama na kusema kuwa, hali imekuwa ngumu.

Gallant pia alimwambia Netanyahu kwamba “vitendo vya upande mmoja katika mfumo wa mahakama lazima vikomeshwe”; Kwa sababu suala hili limekuwa na taathira kubwa kwa vikosi vya akiba vya jeshi la Kizayuni na jamii ya utawala huu.

Benny Gantz, Waziri wa zamani wa Vita wa Kizayuni amesema leo kwamba, kutekelezwa pendekezo la mabadiliko ya muundo wa Kamati ya Uteuzi wa Majaji kutazuia kupatikana suluhu kuhusu mpango wa kudhoofisha mfumo wa mahakama katika utawala huu.

Gantz aliwataka wale ambao ni wagombea wa nafasi ya jaji katika Mahakama ya Juu ya Kizayuni kufuta ugombeaji wao. Alisisitiza: “Hakuna kitu kama suluhu la upande mmoja. Katika suluhu, wahusika wanajadiliana pamoja. Tunataka kuanzisha mazungumzo yanayotokana na mpango wa Isaac Herzog (mkuu wa utawala wa Kizayuni) kuchunguza mageuzi ya kina.

Yair Lapid, kiongozi wa upinzani wa Kizayuni, alisisitiza kuhusu pendekezo jipya linalohusiana na uteuzi wa majaji wa baraza la mawaziri: “Hili si suluhu [la mgogoro], bali ni utawala wa wanasiasa dhidi ya mfumo wa mahakama.”

Mwezi Januari mwaka huu, baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni likiongozwa na Benjamin Netanyahu liliwasilisha mpango wa kurekebisha mfumo wa mahakama wa utawala huo. Netanyahu, ambaye amekuwa mahakamani kwa miaka mingi kwa tuhuma za rushwa, hongo na usaliti wa uaminifu, anapanga kutoroka kutoka kwa kesi hiyo na kile anachokiita “mageuzi ya kijeshi ya mahakama”.

Kufuatia uamuzi huu, kwa wiki ya kumi na moja mfululizo, maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu yameshuhudia maandamano makubwa kupinga mpango huu. Mamlaka za utawala wa Kizayuni zinatahadharisha kwamba mvutano huo katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu unaweza kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kuhusiana na hilo, “Tamir Pardo”, mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi la Kizayuni hivi karibuni katika mahojiano na Kanali 12 ya utawala wa Kizayuni akigusia maandamano ya maelfu kadhaa ya watu na mizozo ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kusema kuwa, Israel haihitaji. Iran kuangamizwa, kwa sababu tayari ni Kujiangamiza ni moja kwa moja.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *