Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuwa, mgogoro wa kupanda gharama za maisha nchini Uingereza unaweza kuzidisha kiwango cha wanawake wanaokufa wakati na baada ya ujauzito.
Ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani inaonya kuwa, hali hiyo inashuhudiwa, huku ukosefu wa usawa wa kiafya ukizidi kuwa mbaya zaidi na kwamba, akina mama wajawazito wanatumbukia katika umaskini.
Aidha inaelezwa kuwa, asilimia 9.6 ya akina mama wajawazito nchini Uingereza katika kila watoto laki moja wanaozaliwa, huaga dunia wiki sita tu baada ya kujifungua.
Dk Natasha Azzopardi-Muscat, mmoja wa maafisa wa WHO na daktari aliyebobea katika afya ya uzazi nchinii Uingereza, anasema kuwa, kuna “uhusiano unaoonekana” kati ya uwezekano wa mwanamke kufa katika wiki za awali kabla na baada ya kujifungua na kiwango cha juu cha umasikini.
Ameongeza kusema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) lina wasiwasi sana na hali ya wanawake nchini Uingereza hasa kutokana na kupanda pakubwa gharama za maisha na kwamba, hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi katika siku za usoni.
Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, takwimu zinaonyesha kuwa Uingereza ndiyo nchi ghali zaidi yabarani Ulaya kuishi kutokana na matatizo makubwa ya kiuchumi na kifedha yanayoikabili nchi hiyo.
Inaelezwa kuwa, ongezeko kubwa la mfumuko wa bei kuwahi kushuhuhudiwa huko Uingreza na ongezeko lisilozuilika la gharama za maisha nchini humo zimeiweka nchi hii katika hali mbaya zaidi ya kiuchumi katika nusu karne iliyopita.