Wimbi jipya la maambukizi ya Corona latazamiwa Ufaransa.

Mshauri wa ngazi ya juu wa masuala ya sayansi wa serikali ya Ufaransa ametahadharisha kuhusu ongezeko la wimbi jipya la maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu litakalosababishwa na aina mpya ya kirusi cha corona.

Akizungumza katika mahojiano na redio ya RTL ya Ufaransa, Jean- Francois Delfraissy ameeleza kuwa, maambukizi mapya ya kirusi cha corona aina ya BA.5 yatashuhudiwa nchini Ufaransa mwishoni mwa msimu wa mapukutiko.

Wakati huo huo Ufaransa imeripoti kesi mpya za maambukizi mapya ya COVID-19 zipatazo 124,724 katika muda wa saa 24 zilizopita. Jumla ya maambukizi 147,000 ya COVID-19 yaliripotiwa juzi Jumanne pekee huko Ufaransa. Baadhi ya vyombo vya habari vimetangaza kuwa, Ufaransa inatarajiwa kukumbukwa na tsunami mpya ya maambukizi ya corona.

Wengi wanaougua sasa huko Ufaransa ni wale waliopatwa na maambukizi ya kirusi cha corona aina na Omicron. Serikali ya Ufaransa tokea katikati ya mwezi Machi mwaka huu iliweka kando aghalabu ya protokali za kiafya za kujilinda na maambukizi ya corona.

Wiki hii Serikali ya Ufaransa ilieleza kuwa ni lazima kutumia barakoa katika maeneo yenye msongamano wa watu ili kuzuia msambao wa corona. Idara ya Afya ya Umma ya Ufaransa aidha imesisitiza katika ripoti yake ya kila wiki kwamba, kuenea maambukizi ya corona katika miji mikubwa ya nchi hiyo kunaambatana na ongezeko la wagonjwa wapya wanaolazwa hospitalini.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *