Wizara ya Afya ya Gaza ilitangaza kusambaratika kabisa kwa mfumo wa afya katika eneo hili

Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza ilitangaza kusambaratika kikamilifu mfumo wa afya katika hospitali za Ukanda wa Gaza na kuripoti kuwa idadi ya mashahidi wa Kipalestina imeongezeka na kufikia watu 5791.

Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza, Jumanne hii alasiri, ilitangaza ongezeko la idadi ya mashahidi wa Kipalestina na kuporomoka kabisa kwa mfumo wa afya katika eneo hili.

Wizara ya Afya ya Ghaza ilitangaza kuwa utawala huo ghasibu ulizishambulia familia za Wapalestina mara 47 katika saa zilizopita, na matokeo yake watu 704 waliuawa shahidi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya mashahidi wa Kipalestina kufuatia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni imeongezeka na kufikia 5,791, ambapo 2,360 ni watoto na 1,292 ni wanawake.

Mounir Al-Barsh, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Palestina, katika mahojiano na idhaa ya “Al-Mayadeen”, alitangaza kuwa vituo vya matibabu katika eneo hili havijapokea “hata kidonge kimoja” kutoka kwa shehena ya kibinadamu iliyotumwa Gaza.

Wizara ya Afya pia ilitangaza kuwa hospitali 12 na vituo 32 vya afya havina uwezo tena wa kutoa huduma, na inahofiwa kuwa vituo vilivyosalia pia havitaweza kutoa huduma baada ya mashambulizi na kukosa mafuta.

Wakati huo huo, msemaji wa Wizara ya Afya ya Gaza alitangaza kuporomoka kabisa kwa mfumo wa afya katika hospitali za Gaza na kuashiria kuwa kuwa wazi katika hospitali haimaanishi kuwa wanaweza kutoa huduma kwa majeruhi.

Wizara hiyo pia ilitangaza mwishoni kwamba wafanyakazi 65 wa matibabu waliuawa shahidi huko Ghaza na magari 25 ya kubebea wagonjwa yalilengwa katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *