Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Palestina imekaribisha hatua ya Jamhuri ya Afrika Kusini ya kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya utawala wa Kizayuni kwa kutekeleza jinai ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya ‘Hague’.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Palestina (Wafa), Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Palestina ilitoa taarifa na kutangaza: Israel ni utawala unaoukalia kwa mabavu na haramu ambao kauli na vitendo vya maafisa wake vimesababisha uharibifu dhidi ya raia katika mji Ghaza, yote hayo yakiwa kama mifano wa mauaji ya halaiki.
Aidha, waliwafananisha watu wa Palestina na wanyama na viongozi wa utawala huo walidhihirisha azma ya utawala huu ya kutekeleza jinai hizi.
Vilevile, walizuia mahitaji ya kimsingi kama vile maji, chakula na umeme, na kuzuia kuingia kwa dawa na mafuta, na zaidi ya hapo kushambulia makazi ya raia wa kawaida, hospitali na vituo vya makazi ya wakimbizi, na kuharibu vinu na matangi ya maji, huu ukiwa kama ni mfumo mwengine katika mipango ya serikali hii kwa ajili ya kuwaua raia hao ambao kando na kulipuliwa kwa mabomu na kukabiliana na mashambulizi ya kijeshi ya utawala huu wamekua wakifariki kutokana na njaa na kiu.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina ilipongeza hatua ya Afrika Kusini na kufafanua kuwa nchi hii na Palestina ni wanachama wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari (CPPCG) au Mkataba wa Mauaji ya Kimbari, na kwamba hatua ya Afrika Kusini inatokana na Kifungu cha 9 katika Mkataba huu pamoja na kukiuka Ibara ya 2 na ya 3 zilipokatika sehemu ya mwanzo wa Mkataba huu. Mkataba wa utawala wa Kizayuni unaendana kikamilifu na majukumu ya nchi wanachama wa mkataba huo wa kuzuia kutendeka kwa jinai hizo.
Katika taarifa yake, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Palestina imeitaka Mahakama ya ‘The Hague’ kushughulikia ombi la Afrika Kusini haraka iwezekanavyo ili kuzuia mauaji ya umati ya watu wa Palestina. Aidha amezitaka nchi zinazofungamana na utawala wa Kizayuni kuacha kuunga mkono utawala huo.