Waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel ameashiria baraza la mawaziri linaloundwa na Benjamin Netanyahu na kusisitiza kuwa linaonekama kuwa ni baraza la vita.
Waziri wa zamani wa vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel, Moshe Ya’alon, amesisitiza kwamba Israel iko katika hali ya mparaganyiko na utata.
Ya’alon ameongeza kuwa waziri ajaye wa usalama wa ndani wa Israel, Itamar Ben-Gvir ni mtenda jinai ambaye anakabiliwa na mashtaka manane mahakamani ikiwemo kesi ya kuhusika na ugaidi.
Kwa upande mwingine, mtandao wa Kizayuni wa Kan umeripoti kushindwa mazungumzo ya kuunda baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu, kiongozi wa chama cha Likud.
Ripoti zinasema, mzozo wa kogombea mamlaka ya wizara kadhaa katika serikali ijayo ya Israel ulipelekea kiongozi wa chama cha Shas, Aryeh Deri, kujiondoa katika kikao hicho na kuzusha malumbano makali na Bezalel Yoel Smotrich, mkuu wa chama cha Religious Zionist Party.
Awali, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas aliyataka makundi yote na wananchi kuchukua hatua kukabiliana na baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu na kukwamisha njama zake.
Baraza jipya la mawaziri la Israel linajumuisha wanasiasa wenye misimamo mikali ya kifashisti ya mrengo wa kulia suala ambalo limeibua wasiwasi mkubwa ndani na nje ya Israel kwenyewe.