Yemen yakasirika baada ya UAE kuwaingiza ‘watalii’ wa Israel kisiwani Socotra

Hasira zimeenea miongoni mwa watu wa Yemen baada ya kuenea picha zinazowaonyesha “watalii” kutoka utawala haramu wa Israeli wakitembelea kisiwa cha kistratijia cha Yemen cha Socotra ambacho kinakaliwa kwa mabavu na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

aarifa zinasema UAE ndiyo iliyowaingiza ‘watalii’ hao Waisraeli katika kisiwa hicho cha Yemen. Picha zimesambazwa zikiwaonyesha Waisraeli hao wanaodaiwa kuwa eti ni watalii wakipanda milima ya Socotra wakiwa wamevaa bendera za utawala haramu wa Israel.

Wanaharakati katika mitandao ya kijamii wanasema Waisraeli hao wanalindwa na askari wa UAE wakati wote wakiwa Socotra huku wakipeperusha bendera za utawala wa Kizayuni wa Israel kwa makusudi ili kuibua hasira za Wayemeni.

Mwezi Mei mwaka jana Serikali ya Wokovu wa Kitaifa yenye makao yake Sana’a ililaani vikali hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu kuwaingiza Waisraeli katika Kisiwa cha Socotra. Taarifa hiyo ilisema UAE inakiuka sheria za kimataifa kwa kuzingatia kuwa Socotra ni kisiwa cha Yemen kinachokaliwa kwa mabavu na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudia.

Socotra ni kisiwa chenye wakazi 60,000 katika eneo muhimu la baharini la Lango Bahari la Bab el Mandeb ambalo linaunganisha Bahari ya Sham na Ghuba ya Aden pamoja na Bahari Arabu. Taarifa zinadokeza kuwa UAE ikishirikiana na utawala haramu wa Israel inalenga kujenga kituo cha kijasusi katika kisiwa hicho cha Yemen.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *